Tusitegemee kuwaona yamoto band kwenye kazi ya pamoja

Tusitegemee kuwaona yamoto band kwenye kazi ya pamoja

Na John Simwanza

Tafakari yangu ndio iliyo nisukuma na kuamua kuandika Makala hii, ambayo huenda ikaungana na mawazao ya wengi kwa sasa juu ya kundi ambalo lina/lilikua umaarufu mkubwa na limefanya mengi mno katika muziki huu wa kizazi kipya.

Lakini pia kundi hili liliweza kuwavutia na kuwashawishi vijana wengine kutengeneza Band zao kwa kutumia aina ya uimbaji na uwasilishaji wa kazi kwa aina ya Yamoto Band.

Mfano halisi ni kwa band ya Ruby Band ambayo ina vijana wanne kama ilivyo idadi ya wasanii wanao tengeneza Kundi la Yamoto Band.

Yamoto Band ndiyo band pekee ya vijana walio na umri unaoendana kuwahi kuanzishwa hapa nchini. Hakuna asiyejua uwezo wa yamoto Band kuanzia utunzi, uimbaji na hata katika majukwaa mbalimbali ambayo tayari wameshapanda kwaajili ya maonesho mbalimbali.

Hizi ni kumbukumbu tosha katika maisha yao kila mmoja kama yamoto band na pia ni kumbukumbu kubwa kwa Muziki huu wa Kizazi kipya hata kama wasipofanya tena kazi ya pamoja kumbukumbu yao itaendelea kubaki pale pale kutokana na waliyo yafanya katika uwanja wa muziki hapa Nchini.

Kwa kuwa walikutana  na kutengeneza kundi wakiwa wanne hiyo inaashilia kuwa kila mmoja anakipaji chake na uwezo wake binafsi  nje ya kundi.

Na kila mmoja anakila sababu au uhuru wakuonesha alichonacho na ndiyo maana baadhi yao  tumeweza kuwaona wakishirikishwa katika kazi za wasanii wenzao na wakati mwingine wanaonekana katika kazi  zao binafsi.

Miongoni mwa sababu kubwa hasa iliyonipa nguvu yakuandika juu  jambo hili huwenda tusiwaone tena yamoto  band katika kazi za pamoja kama ilivyo kuwa hapo awali ni swala la wao kutokuwa na majibu sahihi juu ya umoja wao hasa wa kikazi baada ya kuona ujio binafsi wa kazi zao ukiwa unaendelea kila leo. Na huku wakifisha uhalisia wa kutokuwa sawa na bosi wao Saidi Fella.

Mpaka sasa dalili zinaonesha wazi kuwa  kila mmoja anaweka jitihada zake binafsi katika kazi binafsi na kutaka kujitambulisha Zaidi.Na huu ndiyo huenda ukawa mwisho wa yamoto Band na kukawa ndio mwanzo wa Aslay,Enock Bellah,Beka flavor na Maromboso kama wasanii wanaojitegemea sio tena kama wasanii ambao wanasimama kama kundi.

Uhitaji wa kazi zao kama kundi bado ni mkubwa mno, kwani tayari mashabiki wengi wanahitaji kuwaona wanakuja vipi lakini kutokana na huu muendelezo wa utokaji wa kazi binafsi unawashtua wengi na kuwaacha mashabiki njia panda wakiwawamejawa na maswali yasiyokuwa na majibu na kila mmoja wao amekuwa mgumu kuweka wazi yaliyomo ndani ya Umoja wao kama Yamoto Band.

Ila ukweli utawaweka huru mno ila kificho kitazidi kuwatumbukiza shimoni kwa maana akili za mashabiki basi zipo katika uwepo ya Yamoto Band na sio msanii mmoja mmoja kama wanavyotoa kazi zao bila kuwa na maelezo ya kujitosheleza.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa