SNURA AMUOMBEA MSAMAHA SHILOLE

11072334_1633038610267322_8261702769367784156_n
Ni siku chache zimepita tangu Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kutoa barua ya onyo kwa msanii Shilole, baada ya picha zake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuoneshsa akiwa maungo wazi kwa bahati mbaya akiwa jukwaani nchini Ubelgiji.
Kwa upande wa Snura, ameonesha kuguswa na tukio hilo kutokana na watu wengi kumpambanisha muda mwingine na Shilole, kulingana na aina ya muziki wanaoufanya.
Snura, amesema kuwa ukweli yeye binafsi kutoka kwenye moyo mwake anamuombea sana msamaha kwa watanzania na jamii kwa ujumla na kuwataka watu wasimuangalie hivyo ambavyo wanamuangalia kwa sasa kama amefanya kwa makusudi.
Ameongeza kuwa ile ni kama ajali hivyo wamuelewe kama ambavyo mwenyewe amesema yule ni mtu mzima na ana maumivu yake ndani ya moyo na kudai kuwa watu wanapozidi kumkandamiza ni kama kuzidi kumuumiza kikubwa ni kumsamehe na kuona kama tukio kama hilo litatokea tena.
SOURCE.BEN Kalonga