“Nikki wa Pili ni maana halisi ya muziki biashara”

“Nikki wa Pili ni maana halisi ya muziki biashara”

Ukijua tofauti ni lazima ufanye yenye utofauti na wakati wote matokeo huja tofauti maana katika uhalisi wewe utakuwa tofauti hivyo tofauti itakuwa na wengi ambao wako tofauti.

Kufikiri tofauti juu ya bidhaa yako ni maana ya kuwa tofauti katika soko lenye ushindani tafauti wa bidhaa nyingi tofauti. (Muziki)

Hivyo hatuwezi kufunga vinywa vyetu wala kuweka peni zetu chini katika kuhubiri kweli ambayo iko tofauti na utofauti ambao sasa upo kwenye muziki wetu.

Tunaposema Nikki wa Pili ni maana halisi ya muziki biashara ni kwa maana ya kuwaza kitofauti kwa wazo kuu la biashara.

Utofauti ni katika tofauti ya utunzi kwa maana katika muziki wa sasa ni wazi wasanii wamekosa na kushindwa kufanya nyimbo zenye maudhui.

Hivyo Nikki amejua akienda tofauti ni wazi atakuwa tofauti katika biashara yake, ni hiki ndicho ambacho kimefanya kuweza kuonekana tofauti na wimbo huu tofauti.

Na nyakati zote waswahili hunena “Hakuna Zaidi mbovu” Kwa maana ya uhalisia wimbo huu umeweza kushika mapema katika masikio ya wengi kwa maana unausikivu tofauti na tungo nyepesi ambazo zimetawala sasa kutoka kwa wasanii wengi tofauti. (Kuwaza Zaidi)

Kweli itatufanya tuwe huru nyakati zote, wimbo huu wa hesabu ni wimbo ambao sasa umetimia kuitwa bora kwa maana ya tungo, Mdundo na midondoko.

Lakini mnogesho wa kiitiko kutoka kwa mtayarishaji mchanga S2kizzy ameweza kukoleza utamu huu wa kwenye sikio, lakini mwamba Joh Makini anaonyesha namna ambavyo yeye ni mwamba tofauti katika kufanya tofauti kwenye kila wimbo ambao atapika.

Na wakati wote waswahili husema “Jina jema hung’ara gizani”. Kuwaza tofauti katika biashara itafanya uifanye tofauti, yafaa ubadilike kulingana na wakati maana nyakati pia hubadiliki.

Tafakari…!

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa