Microphone ni wimbo wa 5 kuwakutanisha tena Ay na Fid Q

Microphone ni wimbo wa 5 kuwakutanisha tena Ay na Fid Q
Nyakati za kusherehesha ujio wao mpya wa wimbo wa Microphone hatukuwa na mashaka na wazee hawa. Maana wote ni bora katika midondoko yenye kuonyesha ukomavu wa kisanaa kila iitwapo leo.

Lakini nogesho jema na zuri ni mdundo toka kwa mtayarishaji bora wa nyakati zote Hermy B,  hakika uviko wa mashairi ya wazee hawa umeleta ladha tamu ya muziki.

Na huu ni wimbo wa 5 kwa Ay na Fid Q kufanya pamoja au kukutana katika wimbo mmoja. Ambapo upo wimbo kama ni Shimo Limetema, Mikono Juu, Jipe Shavu, Upo Hapo na sasa Microphone.

Na kuhusu Microphone ni wimbo wenye ujazo tosha wa wimbo kwa maana ya upana mdundo, usikivu, mashairi na chagizo la midondoko katika ladha mchanganyiko.

Ni wazi ‘Microphone’ ni moja ya nyimbo bora za kushirikiana katika nyakati hizi (2018). Ikumbukwe nyakati hizi ni nyakati za audio mbaya na video nzuri, lakini wimbo huu upo katika ukamilisho wa yote mazuri.

Audio nzuri na video nzuri kwa hakika na hakika.

#TuzungumzeMuziki