Je! Fid Q ni msanii mkubwa asiejielewa? Sehem ya I

Je! Fid Q ni msanii mkubwa asiejielewa? Sehem ya I

Mswahili hakosei katika semi zake maana kwa hakika imetimia sasa yakuwa “Kwenye miti hakuna wajenzi”. (Uhalisi).

Na huu ni uhalisi wenye uhalisia wa msanii Fid Q ambapo wajuzi wanaamini yakuwa ndiye tumaini la mashabiki wote wa hiphop katika nyakati hizi. Na hii ni katika uwepo wake kwa utoaji wimbo au kutokutoa.

Sifa nyingi wajuzi humpa Fid Q kila iitwapo siku tena katika uwazi bila kujali mapokeo ya wasanii wengine. Na ufahari mkubwa kwa Fid Q ni kutokana na sifa za wajuzi wa muziki.

Nasi tunaamini kwa hakika yakuwa “Fahari mama wa ujinga” na hii ni katika simamio la uisho wetu wa Kiswahili wa kila iitwapo leo.

Wajuzi wa muziki hawaachi kunena maneno makali juu ya Fid Q kila mara katika vikao vingi tuketivyo. Mosi ya semi mbaya ambayo masikio yetu hayatamani kusikia ni semi ya “Fid Q ni msanii mkubwa asiejielewa”.

Na wajuzi wamekuwa wakinena semi hii mara kwa mara, lakini pia hutuliza nyinyi (Sisi Tizneez) nyakati zote si mnanena kweli yenye kweli? Mbona sasa hamneni juu ya Fid Q katika uhalisi wa muziki na biashara yake?.

Hakika imepasa tunene tena kwa upana mkubwa ikiwa ni katika mlengo wa kujenga kesho yenye maana na faida kwa Fid Q.

Kauli ya wajuzi wa muziki yakuwa “Fid Q ni msanii mkubwa asiejilewa” ina ukweli kwa wajuzi wote, lakini vipi kwa mashabiki?. Nao wanasadiki yakuwa Fid Q ni msanii mkubwa asiejilewa?.

Itaendelea……

#TuzungumzeMuziki