Vigezo walivyokuwa wanavitaka watayarishaji wa zamani kwa msanii ili aweze kurekodi

Vigezo walivyokuwa wanavitaka watayarishaji wa zamani kwa msanii ili aweze kurekodi

Na John Simwanza.

Muziki huu wa kizazi kipya umeanzia mbali mpaka kufika hapa ulipo. Sisi kama Tizneez tuna kila sababu ya kukupa mambo kadha wa kadha ili kuhahikisha tunailinda kauli mbiu yetu ya “Tuzungumze Muziki”.

Kwa vile leo ni Alhamisi basi acha turudi nyuma kidogo ili uweze kupata machache ambayo yalikuwa yanafanyika katika Muziki. Pengine wakati huu  mambo hayo yakawa hayapo kabisa au yapo lakini ni kwa uchache.

Kuanzia Miaka ya 1990 kuja katika miaka ya 2000 na kuendelea mpaka 2003 mpaka kuja kufika 2005 watayarishsji wa muziki walikua wana utaratibu wao wa kumrekodi msanii bila kuangalia anapata kipato gani kutoka kwa msanii ambae anarekodi wimbo huo.Hali hiyo ilipelekea kuwepo kwa wasanii wachache ukilinganisha na miaka ya hivi sasa .

Watayarishaji wengi walikuwa wanaamini zaidi katika kipaji kwanza kutoka kwa msanii husika na sio pesa. Wasanii wengi kwa wakati ule hasa wenye vipaji walikuwa wanapata nafasi kubwa ya kurekodi, na kufikia hatua yakufanya kazi wakiwa chini ya usimamizi wa Studio (label). Fursa hiyo ilikuwa inawaangukia hasa wasanii wenye Vipaji vya hali ya juu.

Watayarishaji waliokuwa wapo kwa kipindi kile walikuwa wanazingatia uandishi wa mada ambao ndiyo ulikuwa uandishi wa ushindani kwa wakati ule.

Kwaiyo ilikuwa ili uweze kuwa msanii mkali na ukubalike na mtayarishaji Ilikuwa ni lazima uandishi wako uwe unazingatia mada.

Suala hilo ni Tofauti  hasa kwa wakati huu ambapo wasanii  walio wengi wanaimba bila kubadili Mada. Ni Wasanii wachache ambao walikuepo tangu Zamani wanaotumia uandishi huu wakuzingatia mada katika tungo za nyimbo  zao.

Kipaji na uandishi ambao unazingatia mada ulikuwa hauna nguvu yakumshawishi mtayarishaji ili aweze kukuingiza katika Chumba cha kurekodia (Booth Room).

Bali nidhamu ilipewa nafasi kubwa katika maisha ya Sanaa ya muziki kwa wakati ule.  Hivyo Nidhamu lilikua linazingatiwa na watayarishaji wa muziki kwa wakati ule.

Ndiyo mana muziki wetu wa zamani Ilikuwa una kazi nyigi nzuri na kila msanii alikuwa ana nafasi kubwa ya kazi zake kuchezwa katika vituo vya Radio na Runinga.

Hata Uuzwaji wa Album za  wasanii ulikuwa unawalipa kutokana na Ubora wao wa kazi ambazo zilikua zinaishi kwa muda mrefu  Tofauti na kazi ambazo zinafanywa na wasanii wapya au wasanii ambao hawakuepo wakati ule muziki ulipokuwa unazingatia uandishi, kipaji na nidhamu.

Swala hili la watayarishaji wa zamani kuwa na utaratibu huu wa kuzingatia mambo ambayo tumeyazungumzia hapo juu ilikuwa inawasaidia wasanii na  imewajenga wengi.

Na wasanii ambao wanaishi katika mfumo huo ndiyo wasanii ambao wameweza kubaki katika uwanja huu wa muziki wa kizazi kipya wenye mikiki ya kila aina sasa.

Kwa Maandiko haya na mengine mengi yanayo husu game yetu ya zamani utakuwa unayapata kupitia Hapa hapa Tizneez Kila siku za Alhamisi,

 

Kuzungumza Muziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa