THROBACK NA SOGGY DOGGY

THROBACK NA SOGGY DOGGY
Soggy
Ni moja kati ya wasanii wa mwazo waliosaidia kukua na kuenea kwa muziki wa bongo fleva/hiphop.
Nyimbo kama kibanda cha simu ni moja pia ya zile nyimbo zake bora za wakati wote. Nyakati zinakwenda wakati wengi wakitumia muda mwingi kujaribu kufuata historia ya muziki wa hiphop/ bongo fleva ilipotoka, team tizneez inakuja na utofauti ambapo sasa kila alhamis utapata wasaa wa kufahamu msanii mmoja au wimbo wake au hata historia yake kwa ufupi tu kuanzia zamani ambaye alifanya mengi yaliyo jenga huu muziki ambao leo imekuwa ajira ya walio wengi.
Leo katika tab hii ya Throback tupo na mkali Soggy ambaye sasa amejikita zaidi katika tasnia ya utangazaji, ambapo kwasasa yupo maeneo ya Mtwara katika radio moja akiendeleza shughuli zake za utangazaji.
Soggy Doddy katika historia ya muziki wa Tanzania yani Bongo Fleva,Hiphop huwezi kuacha kutaja jina lake kama msanii mkongwe, katika muziki wake alibahatika kutoa album 5 ambazo ni, Album ya ILALA ilifanyika 1997 katika studio za Mj Osterbay ila katika album hii beats zote alitengeneza Prof Ludigo.
Album iliyofuata ilikuwa ni Bongo Newyork mwaka 1999 hii nayo ilifanywa na producer Casto ambae baada alipata matatizo ambayo yakampeleka jela na kutumikia kifungo cha miaka 10, album hii ilitengenezwa katika studio za Fm.
Tupo pamoja ni album ya tatu ya mkali Soggy Doggy Hunter, album hii ilifanywa na producer bora nyakati zote P Majani ndani ya Bongo records nah ii ilikuwa ni mwaka 2000.
2004 ilifuata album ya Niite Chief Rumanyika ambayo hii nayo ilifanyika ndani ya Bongo Records chini producer Majani.
March 11 hii ni album ya mwisho ya Soggy kutoa mpaka sasa hajatoa tena album zaidi ya nyimbo kadhaa.hii ilitoka mwaka 2006 lakini album hii ilikuwa ni tofauti na nyingine maana ilifanyika katika studio tofauti tofauti ikiwa ni tofauti na album za awali.
Leo tumemtazama Soggy na album zake, ni vyema kuwapa heshima wasanii waliochonga njia ya muziki huu wa kizazi kipya. Tutunze historia zao.
Team tizneez inakupongeza Soggy Doggy, tunaheshimu na kujali mchango wako kwenye huu muziki wa bongo fleva/hiphop

soggy-dogy
www.tizneez.com
Twitter tizneez
Facebook tizneez
Instagram tizneez
Youtube tizneez