THROBACK NA LADY JAYDEE #NaamkaTena

jay-dee

THROBACK NA LADY JAYDEE #NaamkaTena

Hii kawaida kwa team tizneez kukuletea kumbukumbu zilizo nyingi zilizofanywa na wasanii wetu wa zamani, ambao wengi wao sasa wameonekana kutopewa heshima na baadhi ya watangazaji walioibuka ambao ni wazi wameendelea kupindisha na hata kutaka kufuta historia iliyoko.

Lady JayDee, a.k.a Komando, Anaconda, Binti Machozi ni msanii pekee wa kike katika muziki wa bongo fleva ambaye tangu atoke kimuziki ameweka rekodi za kipekee, kuna mengi aliyofanya hivyo ni wazi anastahili pongezi.Pia ni msanii ambaye amewafanya wasanii wengi wa kike katika kizazi hiki cha sasa kuimba, licha ya wengi kutosema sasa kwa kukosa ujasiri.

Kwanza ni msanii pekee wa kike katika bongo fleva ambaye ana album nyingi kuliko msanii yoyote yule, album yake ya kwanza ilitoka mwaka 2000 ambayo iliiitwa Machozi, album ya pili ni Binti mwaka 2003, muendelezo wa utojai album uliendea na hata 2005 kutoa album ya Moto, na wakati mwaka 2007 kufutaiwa na album ya Shukrani.

Kipindi kirefu kilipita hapo tangu mwaka 2007 mpaka mwaka 2012 ilipokuja kutoka album ya The best of lady Jaydee, na baada 2014 kufuatiwa tena na album ya Nothing but the truth, ambayo album hii ilizua mambo mengi kuhusu maisha yake na hata kuandika waraka ambao uliwastua walio wengi kuhusu kituo cha radio na mmiliki wake.

Licha ya album pia Lady Jay dee ameweza kushiriki na kushinda katika tuzo nyingi za kimataifa kuliko msanii mwingine wa kike, pia tuzo za ndani ya nchi amekuwa kinara wa kuongoza.Lakini pia ni msanii wa kike mwenye kujiamini maana katika uhalisia amepambana na mengi katika muziki huu, licha ya kuweza kuandaa show zake ambapo ni wazi wengi wasanii wa sasa kwao ni changamoto kuweza kuandana maonyesho yao binafsi, isipokuwa wengi wamekuwa wakisubiri kupata show.

Give me love ni wimbo wake wa mwisho kutoka mwaka 2015, ambapo tangu hapo amekuwa kimya mpaka mwaka huu 2016. Lakini sasa ameanza kuhesabu siku za kurudi katika muziki wake huku akitumia #NaamkaTena ambayo imeonekana kupewa support na watu walio wengi, kuanzia mashabiki na hata wadau muziki pamoja na baadhi ya wasanii wenzake.

Team tizneez Inakutakia kila la kheri katika kuamka tena, sisi tunaamini katika kipaji chako.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez