Perfume album ya Joslin imetimiza miaka 15.

Perfume album ya Joslin imetimiza miaka 15.

Huwezi kutaja wasanii wakali na bora kuwahi kuwepo/wapo katika ardhi ya Tanzania bila tajo la Joslin. (Naam)

Uwezo wa kuchana na kuimba umefanya awe na heshima kubwa mbele ya wajuzi wa muziki. (Kabisa)

Uimbaji wake na kuchana kwake Joslin hakika ni wa mbele ya muda. (Hakika)

Na leo tumekuwa na angalio la “Parfume album” ambapo 2019 album hii inatimiza miaka 15 tangu kutoka kwake. (Miaka)

Ikumbukwe album hii ilitoka mwaka 2004 kabla ya mitandao. Lakini jazo la ubora liko pale pale tangu toka mpaka sasa. (Ndiyo)

Album hii ilikuwa na nyimbo 12 ambapo katika sikivu hukuwa waweza kurusha wimbo hata mmoja. (Wakubwa wanajua)

Side A :

 1. Niite basi

  1. Perfume 
  2. Mtoto wa kiafrika Feat Unique Sistaz

 4. Kwanza 

  1. Namba yangu Feat Q Jay

 6. Simuelewi Feat Juma Nature 

Side B:  

  1. Niite basi remix Feat Albert Mangweair 

 2. Niwe nawe Feat Anet

  1. Sister du Feat Chid Benz 

 4. Nimetoka kwa taabu 

  1. Maisha ft Nuruelly 
  2. Mshikaji mmoja hivi 

Na wapishi wakuu wa album hii ni Jason na Master Jay. Hakika muziki utaishi bali matendo yatapita.

#MuzikiNiSisi