Miaka 18 ya Album ya Daz Nundaz na ujazo ule ule. (Muziki

#TizneeThrobackMusic

Miaka 18 ya Album ya Daz Nundaz na ujazo ule ule. (Muziki)

Ni mwaka 2001 ambapo album ya Kamanda ilitoka rasmi chini ya Bongo Records katika ubora wa P Funk Majani. (Naam)

Ambapo iko wazi Daz Nundaz ni moja ya kundi ambalo limejenga msingi imara wa muziki huu wa kizazi kipya. (Hakika)

Ikumbukwe yakuwa Daz Nundaz inaundwa na wasanii watano ambao ni Daz Baba, Ferooz, Critic, La Rumba na Sajo. (Wakati uliopita)

Na album ya Kamanda ndiyo yenye utakaso halisi katika maisha yote ya muziki huu. Ambapo album hii ilikuwa na nyimbo takribani 8. (Eeh)

Licha ya ubora wa album hii lakini hakuna kumbukumbu halisi ya uuzwaji wake kulingana na mfumo mbovu ambao ulikuwepo. (Soni)

Ila yote ya yote album inabaki kuwa ni album bora ya wakati wote katika muziki huu, kwa maana hutaweza kupeleka wimbo hata mmoja mbele pale ambapo utajipa usikivu. (Hakika)

Tungo zenye kugusa maisha, uimbaji imara wa hisia ni chombezo kuu la kufanya album kubaki kuwa alama haswa katika muziki huu. (Pongezi)

Na nyimbo ambazo zinapatikana katika album hii ni 1. Kamanda

  1. Nitafanya nini
  2. Matatizo Feat Juma Nature
  3. Kioo
  4. Maji ya shingo 
  5. Barua 
  6. Shuka Rhymes 
  7. Barua Remix

Daz Baba anatujuza yakuwa album hii walishirikiana kwa ukubwa mno katika utengenezaji wa album hii.(Umoja)

Lakini umoja wao unafanya mpaka leo hii auwaze kwa maana ilikuwa ni umoja wa hali ya juu. (Upendo)

Hakika “Muziki utaishi isipokuwa matendo” Pongezi kwa Daz Nundaz kwa album hii yenye ladha isiyoisha utamu.

#MuzikiNiSisi