Miaka 12 ya Rado katika usiulize na album isiyo kamili.

Miaka 12 ya Rado katika usiulize na album isiyo kamili.

Mjuzi yoyote atajae nyimbo za hiphop na asitaje ‘Usiulize’ ya Rado basi hapo wajuzi humvua ujuzi.

Na hapo ni katika tajo la nyimbo bila ya zingatio la idadi, hivyo wajuzi wanatupa maana yakuwa ‘Usiulize’ ni wimbo bora wa hiphop katika nyakati zote.

Wimbo huu ulitoka mwaka 2006 ambapo sasa 2018 unatimiza miaka 12. Na mdundo wake ni upishi wa Baucha ndani Baucha’s Records.

Na video ni kutoka kwa Nick Dizzo nyakati hizo ni katika upana wa Bani Vision, hakika nyakati zinakimbia mithili ya upepo.

Upana wa Rado katika uandishi na mitambao ni wa hali ya juu. Kwani mmesahau wimbo wake wa Njia? (2007).

Na album yake yaitwa 18th B.C ambapo ina nyimbo zaidi ya 18. Ila ajabu ya album hii haijawahi kutoka na ipo na ukamilifu tangu 2009. (Ukamili)

Ukimya wa Rado katika upana wa Media ni mkubwa mno, lakini wajuzi huendelea kuburudika na nyimbo zake nyingi.

Ila uwepo wa mara kwa mara katika vilinge vya hiphop umekuwa faraja kubwa kwa wajuzi wengi.

Chem Chem ni msemo wake lakini mfano wa kundi katika upana nje ya Viraka katika mwanzo wa kuchipuka kwake na muendelezo wa sasa.

Hakika wimbo wenye ubora na ubora utaishi nyakati zote. ‘Usiulize’ inabaki kuwa wimbo bora wa hiphop katika nyakati zote.

Lakini deni la album lapaswa lilipwe na Rado lakini yapasa arudi kwa mapana katika uwanja muziki ili aweze kuuza vyema sasa.

#TuzungumzeMuziki