Miaka 11 ya album ya Bomaa Mipango ya D Knob katika ujazo ule ule.

Miaka 11 ya album ya Bomaa Mipango ya D Knob katika ujazo ule ule.

Masikio yetu yamepata usikivu mzuri tangu kuamka kwetu siku ya leo. Na album ya ‘Bomoa Mipango’ ndiyo ambayo imeweza kutupa ladha yenye raha katika usikivu.

Hisia zinarudi nyuma kiasi tunajiona tu mwaka 2008 nyakati za uzao wa album hii.

Hatuwezi kutaja album bora na kusahau album ya ‘Bomoa Mipango’. Na hii inaleta maana yakuwa ‘Muziki unaishi, isipokuwa hovyo”

Hii ni album ya pili ya D Knob ambapo ushiriki wa Master Jay, Bizman, Jonas unaleta kamilisho katika uzalishaji wa album hii. Lakini uzao kamili umekamilishwa na Mika Mwamba.

Album ya ‘Bomoa Mipango’ ilibeba nyimbo 10, na zote ni zenye ujazo kamili wa kuishi mpaka kesho.

Ingewezekana akiwa na Ray pamoja na Squeezer ni mosi, lakini Kitu Gani alkiwa na Q Jay ni pili.

Dakika tatu inaendeleza ujazo wa album hii ya ‘Bomoa Mipango’ ila wimbo kama Yupi ni Yupi, Juhudi za Msela, Dear Mtoto, Wewe Unasemaje, na Kitu Gani Remix zinafanya usichoke kusikiliza album hii.

Na hatuwezi kusahau wimbo wa ‘Mfalme wa mitaani’. Yupi wa D Knob? mbona mitaa bado inahutaji na bidhaa yake ya usasa? Nini kinaendelea juu yake?

Naam! hakika mitaa inamuhitaji kwa upana D Knob tumekumbuka zile huaahua. Lakini mitambao ya upekee ni jambo pili.

Album hii inatupa maana halisi ya “Dunia bila muziki ingekuwa ni mahala pabaya zaidi”

#TuzungumzeMuziki