kweli mtupu wa mwaka 2002 uliopigwa marufuku mwaka 2017.

Ukweli mtupu wa mwaka 2002 uliopigwa marufuku mwaka 2017.

Ukweli mtupu ni album ya kwanza ya kundi tokea Jiji la Tanga Wagosi wa Kaya. Kundi hili linaundwa na wakali wawili ambao ni Mgosi Mkoloni na Dr John.

Kila alhamis Team Tizneez tumekuwa na utaratibu wa kuandika yale ambayo yalifanywa na wakongwe wa muziki huu ambao wamechangia kukua na kueneza muziki wa kizazi kipya ndani na nje ya Tanzania.

Wagosi wa Kaya waliweza kujipatia umaarufu na kipato kwa kuweza kuimba yale yenye ukweli ambayo ni maisha halisi ya watanzania wote. Album hii ilifanyika katika studio za Mj Record chini ya mikono ya Master Jay.

Jina la album yao ya ‘Ukweli Mtupu’ ni jina ambalo liliendana na kile ambacho kipo katika album hiyo. Mara baada ya kutoka kwa album hii ni wazi kulifanyika kwa tour Tanzania nzima bila mapumziko, hii yote ni kwakuwa mashabiki walipenda ukweli huo.

Mtayarishaji wa album hiyo aliwahi kusema “Nimefanya album nyingi ila album ya Ukweli mtupu ni album ambayo ilibadilisha mambo mengi katika maisha yangu ya muziki.

Katika album ya ‘Ukweli Mtupu’ hakuna jambo ambalo lilifichwa ikiwa ni katika lengo la kuweka mambo sawa katika sehemu ambazo zimezembea.

Ukweli huu wa mwaka 2002 ndio ukweli ambao sasa wasanii wanapigwa marufuku kuimba ukweli huu mwaka 2017.

Album hii ilikuwa na takribani nyimbo  nane. Ambazo nyimbo hizo ni

1.Tanga kunani?
2.Wauguzi ft. First Mack.
3.Titamtambuaje? ft.Lady Q,John Woka
4.Wakulima ft. Ustaadh Muarobaini
5.Vinatia uchungu ft. John woka
6.Mnajua nampenda ft.Mr Paul
7.Tanga kunani? rmx
8.Kero(umeme na maji)

Tuambie wimbo gani ulikuwa unaupenda Zaidi kati ya hizo juu?

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez

Attachment