Kunako 2002 Afande Sele aliyaona ya 2018.

Kunako 2002 Afande Sele aliyaona ya 2018.

Fikra za Mfalme Sele hakika zitaishi milele katika muziki huu. Lakini wasanii wachache mno ambao pia humpinga katika mengi.

Ila kupinga kwao ni kutokana na kutojipa wasaa juu ya kusikiliza mengi yenye maana kutoka kwa Mfalme Sele, hivyo wala tusishangazwe nao. (Kiburi)

Nyakati za kuchangamka kwa muziki huu mwaka 2002 Mfalme Sele aliweza kutoa album ya Mkuki Moyoni.

Ambapo wajuzi hunena yakuwa katika album bora za nyakati zote hii ni moja wapo. Na album hii imebeba nyimbo kama Mtazamo, Mayowe, Habari Kamili, Mkuki Moyoni, Watu na Fedha na nyingine nyingi.

Na Bongo Records chini ya P Majani ndiyo watayarishaji wa album hii.

Na katika wimbo wa ‘Watu na Fedha’ hakusita kueleza hisia zake katika uhalisi wa watangazaj na mapromota.

Ambapo anasema ” Tatizo mapromota na maradio presenter, wachache sasa wanafuata, fani wanaibolonga top 10 za kupanga yani hawajali ubora hata kazi ndizo wanapiga.

Nyimbo za ujinga ujinga ndo kila muda wanatwanga, bila kujali ujumbe ilimradi umekata panga.

Na kama hauna kitu basi utakoma kuringa hili mimi nalipinga japo kwangu afadhali, vipi wasanii wachanga?.

Mbele wataweza songa! thubutu, kama mwendo ndo huu milele hawatasimama, na kama watasimama basi rap itazama”

Hayo amesema mwaka 2002, lakini ndiyo uhalisi wa 2018 katika muziki wetu.

Kiukweli kuna wasanii wengi mno wenye vipaji na nyimbo kali lakini tazamo la watangazaji wengi ni fedha si kazi bora na kipaji.

Imefika hatua yapasa na watangazaji nao “Watosheke na mishahara yao” Lakini wapunguze kuhoji udaku zaidi bali nyimbo katika endelezo la sanaa ya muziki.

Udaku hauwezi kukuza wala kutangaza sanaa ya muziki hata kwa uchache.

Naam! Hekima za Mfalme Sele zikatawale vichwa vyenu.

#TuzungumzeMuziki