Je!Unajua yakuwa BBG ndiye aliyemfundisha Sugu kuandika mistari?

#TizneezThrobackMusic

Je!Unajua yakuwa BBG ndiye aliyemfundisha Sugu kuandika mistari?

Sugu ndiye msanii ambaye ana mchango mkubwa katika muziki wa kizazi kipya ambapo tangu miaka ya 1980 na kuendelea aliweza kuupigania ipasavyo.

Lakini yapasa ujue Dj BBG ndiye mtu aliyemfundisha kuandika mistari ya kiswahili kwa ufasaha Sugu. Na baadae BBG aliacha kurap na kuwa kama Dj wa Sugu katika matamsha mengi mpaka leo hii.

Lakini nyakati hizo miaka ya 1988 mpaka 1990 wasanii waliopenda kurap walitumia lugha ya kingereza na zaidi kukopi nyimbo ambazo zilitamba tokea Marekani.

Na kama msanii atarap kwa kiswahili basi atatumia midondoko ya umarekani. Na miongoni mwa wasanii ambao walitumia midondoko ya marekani ni Saleh Jabir katika wimbo kama Ice Baby ya Vanila Ice na OPP ya Naughty By Nature na hivyo ndivyo ilivyokuwa.

Sugu na kundi lake la Niggaz 2 Public Mbeya, ukitoa kundi ambalo lilikuwa Dar es Salaam ambalo lilikuwa na jina kama hili lakini hili ni kundi lake ambalo lilikuwa likipatikana Mbeya. Na liliundwa na wasanii kama BBG na Sande.

Niggaz 2 Public waliweza kuandaa tamasha lao Jijini Mbeya ambapo ni kundi pekee lilioweza kuwa na nguvu kubwa Jijini Mbeya. Na tamasha lao waliandaa wao kama wao katika miaka hiyo ya 1991-1992.

Na kutokana na muitikio mkubwa wa watu na umaarufu mkubwa wa kundi hilo ulipelekea kupata dili kutoka kwa Shirika la GTZ ambalo ni shirika la misaada chini ya Wajerumani na kuweza kuwalipa vyema Niggaz 2 Public Na Shirika hili lilikuwa likiwatumia katika kampeni zao za UKIMWI na akini Sugu walikuwa wakitumbuiza katika kila upande ambao Shirika la GTZ lilikuwa na kampeni.

#TuzungumzeMuziki Ni wazi Sugu anastahili heshima kubwa katika muziki huu inashangaza kuona leo hii mdau pekee ndiye mwenye kupewa heshima kiasi cha wasanii kujisahaulisha juu ya mengi ambayo Sugu ameufanyia huu muziki ambao leo hii ni ajira kwa wengi.

Ni vyema tumpe/Mumpe heshima yake Sugu maana amepigania huu muziki kwa hali zote.

Source! Sugu The Autobiography

 

#TuzungumzeMuziki

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa