Je!Unajua P Funk Majani alishiriki katika Yo Rap Bonanza 1994 jukwaa moja na Mr II Sugu?

Je!Unajua P Funk Majani alishiriki katika Yo Rap Bonanza 1994 jukwaa moja na Mr II Sugu?

P funk Majani ni moja kati ya watayarishaji bora wa wakati wote wa muziki wa kizazi kipya, ila wengi hawajui kama P Majani ni miongoni mwa wasanii walioshiriki shindao la Yo Rap Bonanza yaliyokuwa yakiandaliwa na promota Kim chini ya kampuni yake Kim and the Boyz ambapo sasa Kim ni marehemu.

Mwaka 1994 ni mwaka ambao Yo Rap Bonanza yalifanyika ambapo ilikutanisha makundi mengi ya Rap wakati huo. Moja ya makundi kati ya yaliyo mengi ni kundi la Majani lilikuwa likifahamika kwa jina la ‘No Name’ ambapo lilikuwa likichana kwa lugha ya kingereza Zaidi.

Na mashindano haya yalifanyika katika ukumbi wa Empress Cinema,baadhi ya makundi shiriki katika shindano hili yalikuwa ni Kwanza Unit, 2proud and Da Young Mobb ambapo kundi hili alikuwepo Mr II Sugu na Hard Blasterz ila hii ni kabla ya Prof Jay kujiunga.

Na Kwanza Unit ndiyo walikuwa washindi wa shindano hilo la Yo Rap Bonanza 1994.

Hii ni #TizneezThrobackMusic

Mwisho.