Je! Wajua yakuwa wimbo wa Kibanda cha Simu umetimiza miaka 15?

Je! Wajua yakuwa wimbo wa Kibanda cha Simu umetimiza miaka 15?

Kibanda cha Simu ni wimbo Soggy Doggy ambao ni wazi ni bora katika nyakati zote.

Na wimbo huu ulirekodiwa mwaka 2003 na kutoka rasmi mwaka 2004, na mtayarishaji ni P Funk Majani ndani ya Bongo Record.

Wimbo huu mpaka sasa una miaka 15 tangu uzao wake, lakini kitu cha kushangaa ni kwamba hata awe amepanda msanii gani katika tamasha, pale ashukapo na kupanda Soggy na wimbo huu hakika mashabiki huamka vyema kwa hali ya juu.

Hii ndiyo maana ya kusema Kibanda cha simu ni wimbo bora wa nyakati zote, ikumbukwe kizazi cha sasa cha mtandao kina ubishi wake lakini si katika wimbo huu.

Mwadada Josephine ni msanii shiriki katika wimbo huu, na sasa hafanyi tena muziki bali yupo na biashara zake nyingine, ilihali ni mama wa familia.

Na wimbo huu wa Kibanda cha Simu unapatikana katika album ya “Niite Chief Rumanyika” Iliyotoka 2004 ambapo wimbo kama Story, Kurwa na Doto na nyingine nyingi zinapitakana humo.

Lakini Soggy ni msanii ambaye ana album nyingi pia, mpaka sasa anazo album 5.

Ni wazi tukizungumza waliochangia kukuza na kueneza Bongo Fleva ni wazi Soggy anapaswa kutajwa tena kwa hali ya ukubwa.

#TuzungumzeMuziki

#TizneezThrobackMusic