Je! Wajua Rama Dee alishinda tuzo ya KTMA 2013?

Je! Wajua Rama Dee alishinda tuzo ya KTMA 2013?

Wajuzi wanaamini yakuwa Rama Dee ni msanii bora wa nyakati zote katika uwanja wa muziki wetu. (Hakika)

Lakini huwezi kujua ubora wa Rama Dee kama huna sikio lenye usikivu juu ya muziki mzuri wenye tungo adhimu na ladha tamu ya uimbaji.

Na kama unategemea kusikia ubora wake kupitia ‘Media’ hilo sahau, maana huko msanii hawezi tajwa kama ni bora mpaka afanye lenye fedheha mbele ya jamii. (Uhalisi)

Lakini kwa wajuzi wa muziki wao wananena yakuwa “muziki pekee umetosha kumpa heshima mbele ya wote wenye kujua namna ya sanaa ya muziki ilivyo”

Na katika kukumbuka kumbukumbu Rama Dee alishinda kwa mara ya kwanza Tuzo ya KTMA 2013 katika kipengere cha wimbo bora wa Rnb.

Ambapo wimbo wake wa ‘Kuwa na subira’ akiwa na Mapacha Maujanja Saplaya (Vinega) ndiyo uliyoweza kushinda tuzo hiyo. Lakini alikuwa akichuana na Belle 9 pamoja na Ben Paul.

Ikumbukwe nyakati hizo Rama Dee hakuwa kabisa ni msanii mwenye kupewa nafasi katika ‘Media’ bali mashabiki walikuwa ni wenye ujuzi wa kujua tofauti ya tofauti ya ubora wa muziki, na sio kama nyakati hizi. (Soni)

Ingawaje wajuzi hunena yakuwa “Huitaji tuzo ili uonekane bora, bali ubora wa wimbo/msanii ni kuwa bora katika wengi na nyakati zote, na simamio la sanaa pekee. (Wajuzi)

Ambapo inaaminika Rama Dee ni moja ya wasanii wenye kazi bora katika nyakati zote, ambaye yeye amesimamia muziki pekee.

Naam! Nasi twanena ni bora katika yote yenye ujazo wa sanaa ya muziki yani tungo, uimbaji na uhalisi wa maisha ya sanaa.

#TuzungumzeMuziki