Je! Unajua Witnes alishinda tuzo ya Channel O 2008?

Je! Unajua Witnes alishinda tuzo ya Channel O 2008?

Witnes si msanii ambaye hutajwa katika wale wachonga barabara vyema ili wengine wapite kiurahisi.

Lakini kwa wajuzi wa muziki hawaachi kunena hadharani yakuwa Witness Kibonge Mwepesi ni moja ya wadada wa hiphop ambao pia wamechonga njia ya wengi kwenda kimataifa.

Ambapo mwaka 2008 na wimbo wake wa ‘Zero’ aliweza kushinda katika tuzo za Channel O.

Ambapo katika tuzo hizo alikuwa akiwania sehemu tatu ambazo ni Best Hiphop Video, Best Callobo/Duo na Best African East Video.

Ambapo wimbo wa ‘Zero’ akiwa na Fid Q ndiyo ambao ulimpa ushindi huo katika sehemu ya ‘African East Video’

Ambapo video hii ni kutoka kwenye mikono ya Adam Juma moja ya watayarishaji bora wa wakati wote.

Tukiacha mengine mengi ya Witnes katika nyakati hizi wajuzi bado wanaamini yakuwa ndiye msanii bora wa hiphop kwa upande wa kike, Midondoko na mistari yeye ni mwenye ujazo tosha.

#TuzungumzeMuziki