Je! unajua wimbo wa Sifai wa Q Jay unatimiza miaka 12 tangu kutoka kwake?

Je! unajua wimbo wa Sifai wa Q Jay unatimiza miaka 12 tangu kutoka kwake?

Q Jay, Joslin na Makamua ni wasanii ambao walikuwa wanaunda genge la Wakali Kwanza.

Lakini genge lao halikuwa na uzio wa kila mmoja kufanya kazi kwa upekee wake, ila kufanya kwa upana wa vile msanii awezavyo.

Ukitamzama Joslin alikuwa mwenye kazi nyingi, Q jay kadhalika Makamua. Na uhalisi wenye uhalisia kwa hakika kazi ziliongea na zaongea mpaka sasa.

Na moja kati ya kazi za Q Jay zenye ubora wa nyakati zote ni ‘Sifai’ ambayo alimshirikisha Joslin.

Ambapo wimbo ulifanyika ndani ya Mj Records/ Twende Kazi Ent. Na wimbo huu unapatikana katika album ya ‘Vipaji Compliliation Album’.

Na video ni usimamio wa Adam Juma katika nyakati Visual Lab

Na mpaka sasa wimbo huu unatimiza miaka 12 tangu kutoka kwake mwaka 2006. Na wajuzi wanaamini yakuwa muziki huu ni bora kwa mambo makuu matatu.

Tungo, uimbaji na mdundo. Kwa upana wa tungo zenye uisho wa uhalisi katika ujazo kamili.

Ila uimbaji wa hali ya juu kwa upana wa Q Jay katika ubora wa sauti yake, ambayo si yenye kupayuka bali utulivu kamili.

Lakini mdundo wenye ukamili lakini changanyo la tungo, uimbaji na mdundo katika usawia wa usafi wa usikivu wenye uonjo kamili wa muziki wenyewe unaleta ladha bora kila usikiapo.

Ni wazi muziki bado unawahitaji wasanii hawa wote maana kwa wajuzi ni wasanii ambao walikuwa mbele ya nyakati.

Hivyo sasa pia ni nyakati zao za kufanya vyema, hivyo kuna kila sababu ya kurejea kwa mapana yao.

#TuzungumzeMuziki