Fahamu wimbo wa Afande Sele maalum kwa mwanae Tunda

Fahamu wimbo wa Afande Sele maalum kwa mwanae Tunda

Selemani Msindi ni moja kati ya wasanii bora wa hiphop wakati wote. Afande Sele alijipatia umaarufu wenye heshima kwaajili ya tungo zake ambazo mara zote hubeba jumbe zenye kuishi kila leo.

Leo ikiwa ni #ThrobackTizneezMusic tumetazama kwa upande wa msanii Afande Sele. Ambapo katika maisha yake ya kimuziki amewahi kumwimbia wimbo mwanae Tunda.

Wimbo huo unaitwa Mwanangu ambao unapatikana katika Album ya Darubini Kali iliyotoka mwaka 2004.

Wimbo huo ulifanyika katika studio za Fm chini ya mtayarishaji Double B. Lakini pia wimbo huo alimshirikisha kijana toka Ghetto Boyz Juma Mjivuni.

Katika wimbo huo licha ya kumwimbia mwanae Tunda ila pia ni wimbo ambao unagusa watoto wote katika jamii, pia wazazi juu ya kutunza watoto wao.

Lakini pia hakuacha kuwakumbusha watoto/mtoto juu kuzingatia elimu katika maisha yake. Ila wazazi hasa vijana si jambo jema kuwakataa watoto ambapo alisema “Ukipitapita ukapata mtoto mtunze ujana ni maji ya moto na yatapoa hata kama mtu hajayatikisa.

Huu ni moja kati ya wimbo bora kwenye muziki wa hiphop ambazo umebeba ujumbe ambao utaendelea kuishi.

Usikilize hapa chini

Facebook Tizneez

Twitter Tizneez

Youtube Tizneez

Instagram Tizneez