Fahamu kuhusu album ya pili ya marehemu Albert Mangweair.

Fahamu kuhusu album ya pili ya marehemu  Albert Mangweair.

2013 ndio mwaka ambao msanii wa muziki wa kizazi kipya  Albert Mangweair alifariki dunia nchini Afrika ya kusini, ambapo alienda huko kwa shughuli zake za kimuziki.

Mpaka  Albert anaondoka kwenye uso wa dunia tayari alishakuwa na Album mbili katika uwanja wa muziki wa kizazi kipya. Album ya kwanza iliitwa A.K.A MIMI, ambayo iliweza kuchukua tuzo ya album bora mwaka 2004 katika tuzo za Kili Music. Ambapo album ilikuwa chini ya usimamizi wa P Majani ndani ya Bongo Records.

Baada ya hapo ukimya juu ya utoaji album juu yake ulikuwa mkubwa, bali wimbo baada ya wimbo ndiyo zilifuata kwa mkali huyu wa mitindo huru.

Mwaka 2010 ndio mwaka ambao aliamua kutoa album yake ya pili.Album hiyo iliitwa N’GE 1982, Mangweair safari hii akiwa chini ya usimamizi wa Tippo (jamaa wa Zizzou Fashions) alidondosha albamu yake ya pili iliyokwenda kwa jina la N’ge 1982 Japo haukusifika kama albam yake ya kwanza lakini ilikuwa moja kati ya albamu bora kabisa.

Baadhi ya nyimbo zilizomo katika albamu hiyo ni.

 • Speed 120 ft Chidbenz
 • Tz hustler
 • Tupo juu ft Squizer
 • Nipe dili ft DarkMaster
 • She performs
 • M.A.F.IA ft Jmo
 • Bonie & Clyde
 • Wa Kitaa ft Babu wa kitaa
 • Bila Muziki
 • Mida mibovu
 • A.K.A mimi
 • Birthday (N’GE)
 • Singida Dodoma
 • Mapenzi gani
 • CNN FT. Fid Q Album hii ilifanyika katika studio tofauti tofauti licha ya nyimbo nyingi kufanyika tena Bongo Records.

Katika album hii upi ni wimbo ambao unaupenda Zaidi?

Mwisho.

Attachment