Fahamu juu ya album ya kwanza ya Juma Nature.

Fahamu juu ya album ya kwanza  ya Juma Nature.

Juma Nature ni moja kati ya wasanii wachache ambao ni vipenzi vya watanzania walio wengi wenye mapenzi makubwa na muziki wa kizazi kipya.

Wakati tukiendelea mbele ya muziki huku wakiibuka wasanii wengine wenye vipaji vya hali ya juu na kuweza kuendeleza muziki mbele, lakini bado Juma Nature anabaki na ubora wake tangu kufahamika kwenye muziki mpaka sasa.

Tizneez inakuletea Throback katika kufahamisha walio wengi juu ya album za wasanii mbalimbali ambazo ziliweza kufanya vyema.

Mwaka 2001 ndiyo mwaka ambao Juma Nature aliweza kutoa album yake ya kwanza ambayo inaitwa Nini Chanzo. Album hii ilisimamiwa vyema na mtayarishaji bora wakati wote ambaye ni P Funk Majani chini yqa Bongo Records.

Katika album hii kuna nyimbo 11 ambazo ni.

1.Kighettoghetto rmx ft Mr.Paul
2.Sonia
3.Wimbi La Njaa rmx
4.Jinsi Kijana
5.Tumepigika ft AY
6.Nini Chanzo
7.Juu Kwa Juu
8.Hili Game ft TID
9.Jinsi Kijana rmx
10.Haya we
11.Wimbi La Njaa 2 rmx.

Katika album hii tuambie upi ulikuwa ni wimbo wako bora?

Tupe maoni yako hapa.