Fahamu Album ya Juma Nature iliyovunja rekodi mwaka 2003.

Fahamu Album ya Juma Nature iliyovunja rekodi mwaka 2003.

Juma Nature ni moja kati ya wasanii waliochangia kukua na kuenea kwa muziki wa kizazi kipya hapa nchini na nje ya nchi.

Huwezi kutaja wasanii ambao waliwahi kuweka rekodi za upekee katika muziki wa kizazi kipya bila kutaja jina la Juma Nature.

Mwaka 2001 ndiyo alitoa album yake  ya kwanza ambayo ilikuwa ikiitwa ‘Nini Chanzo’. Lakini mwaka 2003 pia ilitoka album yake ya pili ambayo iliweza kuweka rekodi katika muziki wa kizazi kipya, album hiyo iliitwa ‘Ugali’ambapo mpishi mkuu alikuwa ni P Funk Majani chini ya Bongo Record.

Uzinduzi wa Album hii ya Ugali ulifanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo Juma Nature aliweza kujaza ukumbi huo. Inaaminika ndiyo msanii wa kwanza kuweza kujaza ukumbi huo.

Album hii ndiyo iliweza kubadilisha maisha ya Juma Nature kiuchumi, maana iliweza kuuza mauzo ya juu. Ingawa mpaka leo bado haijulikani ni kiasi gani cha pesa alipata lakini pia aliuza kopi ngapi katika wiki ya kwanza tu mara baada ya kutoka kwa album. Yote haya ni sababu ya mfumo mbovu ulikouwepo kutoka kwa msambazaji

Katika album hiyo kulikuwa na nyimbo kama,Sitaki demu,Ugali, Salio la vesi, Jela, Aah wapi, Umoja wa Tanzania (feat. Prof. Jay), Hali ngumu, Sitaki demu RMX na Inaniuma sana.

Picha ya Cover ya Album hiyo tazama hapa chini.

Tuambie ni wimbo gani ulikuwa unaupenda zaidi katika album hii ya Ugali.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa