Album ya Lady Jaydee Machozi ilitayarishwa kwa gharama kubwa zaidi mwaka 2000

#TizneezThrobackMusic
Machozi ni album ya kwanza ya Lady Jaydee ambayo ilitoka mwaka 2000. Ambapo muandaaji wa album hii ni Master Jay katika studio za Mj Record.
Na inaaminikia yakuwa hii ndiyo album ya kwanza ya katika muziki wa kizazi kipya kutumia gharama kubwa kwenye utayarishaji katika mwaka huo 2000.

Kupitia album hii kila sikio lenye usikivu wa muziki ulijua Lady Jaydee ni nani katika muziki wa kizazi kipya.

Tazama picha ya album hiyo hapa.

 

Na album hiyo ilikuwa na nyimbo zifuatazo •Machozi (remix) * Nalia * Penzi la milele * Pumziko * Waweza kwenda (Rajabu’s mix) * Nakupenda * Nimekubali (akiwa na Ray C) * Matatizo * Tatiza * Shida * Umuhimu wako * Waweza kwenda (JM mix)

Ni wazi katika uhalisii Lady Jaydee ameweza kuwa kwenye muziki na ubora wa wakati wote maana amejua namna ya kuishi katika miiko ya sanaa.

#TuzungumzeMuziki Hakika Lady Jaydee ndiye msanii bora wa kike wa wakati wote kwenye muziki wa bongo fleva.

Kuna ambaye anaweza kupinga ubora wake?
#TuzungumzeMuziki