Zavara Aingilia kati ya Gadner na Lady Jaydee

Capture
Ramadhani Moonjika wengi wakimfahamu kwa jina la Zavara kutoka kwenye kundi la kwanza Unit ambao ni miongoni mwa makundi yaliosaidia kukua na kuenea kwa bongo fleva/hiphop ndani na nje ya nchi.
Zavara hakusita kuweka hisia zake juu ya kauli iliyotolewa na mtangazaji wa kituo cha Clouds Fm ndugu Gadner Habashi, juu ya Lady Jaydee katika hafla moja ilifanyika usiku wa kuamkia leo.
Ambapo kupitia mtandao wa picha Instagrama Zavara ameandika “Nakemea udhalilishaji alofanyiwa jidada JayDee.
Huu ni mporomoko wa MAADILI wa hali ya juu. Wapi taasisi za maadili ya vyombo vya habari?! Kukalia kimya suala hili ni kulea HULKA za kishenzi na kutapelekea taifa letu mahala pabaya sana.

Jumuia ya wasanii na wadau wengine kama kweli mnajali nataka kuskia mnakemea hili kwa kujumuika huu mjadala. #kemeamporomokoMaadili …: http://youtu.be/aZB5qvFaNPo www.tizneez.com
Twitter tizneez
Facebook tizneez
Instagram tizneez
Youtube tizneez
Tazama picha yake chini