Young Dee Akiri kutumia madawa ya kulevya, ila amkana Tunda.

young-Dee

Young Dee Akiri kutumia madawa ya kulevya, ila amkana Tunda.

Mapema leo katika mkutano na wana habari hakusita kueleza kile ambacho kilikuwa ni fununu ambacho ni wazi hata kilifanya atunge wimbo ulioitwa fununu mwaka jana.

Wimbo huo wa Fununu alizungumza mengi kuhusu mashabiki walio wengi ambao wamekuwa wakimshutumu kutumia madawa ya kulevya.

Lakini katika hali ya kujiamini mapema leo hakusita kusema “Ni kweli nimekuwa nikitumia madawa ya kulevya mpaka sasa ninapozungumza imeshatimia mwaka mmoja na miezi 6. Lakini nimeamua kuacha maana ni wazi sioni faida zaidi ya kuharibu maisha yangu.

Siwezi kumpoint fulani kama eti ndiye ameniingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya ila ni marafiki wengi. Watu kusema Tunda ndiye ameniingiza hilo halina ukweli wowote. Na narudia tena siwezi kusema ni fulani, ila mimi nimeamua kuachana na maswala hayo na nipo tayari kutoa ushirikiano na serikali kama ikihitaji msaada wa mimi.

Lakini pia nichukue nafasi hii kuomba msamaha kwa mashabiki wangu, nawaahidi kufanya mambo mazuri na kuwa mfano bora katika jamii yangu. Pia hakika nipo katika mikono salama ya Label yangu ya MDB. Hivyo watu wategemee mazuri kutoka kwangu.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez