WITNES “SHAA USIWE KAMA WALIOPEWA MASHARTI NA MGANGA”

WITTY

Buku jero ni wimbo wake unaofanya vizuri mkali Witnes ambaye katika video hiyo ameonyesha wepesi wake hasa katika kucheza wimbo huo. Witnes Kibonge Mwepesi ambaye miaka ya nyuma walikuwa pamoja na Shaa katika kundi la Wakilisha pamoja na Marehemu Langa Kileo.Katika kundi hilo la Wakilisha waliwahi kutamba na vibao kama, Hoi,kiswanglishi na nyingine nyingi.Miaka kadhaa baadae kundi hilo lilivunjika kwasababu ambazo zilionekana ni za kimaslahi.Na baada ya hapo kila mmoja akawa anafanya kazi zake binafsi.

Kupitia mtandao wa Instagram ambao umeonekana kuchukua akili za wasanii na watu maarufu zaidi kuwa kama baraza la kueleza matatizo yao, msanii Witnes nae amejikuta akiingia katika mkumbo huo baada ya kuandika kuhusu Shaa ambapo ameandika. “

“Kiukweli huwa mara nyingi sielewi ni kwa nini watu huniuliza kwa kutaka kuconfirm juu ya bifu kati yangu na Shaa. Kwa sababu ni hakuna ila huwa ninawajibu ukweli kwamba hakuna na huwa tunawasiliana kwa simu most of the times though hatuna ukaribu kama kipindi cha mwanzo cha wakilisha,. ama kama msanii mwenzangu ila tuko poa. But ukweli ni kwamba mimi ndo huwa ninampigia simu, kumtext pamoja na kumpa hongera ya nyimbo kadhaa alizowahi toa na mungu ni shahidi wangu, ila tukikutana live tunachekeana vizuri na kufurahiana but Leo nimegundua patakua na vita baridi nisiyoijua. Kwasababu kiukweli Shaa ninampenda sana kama mdogo wangu na ndugu yangu kwetu kumoja. Ila this week nimemtafuta hewani sana tu kiukweli kwa kuwa nimemmiss mno na nilitaka kumuuliza kama we could go out for dinner ama whatever so that we can catch up! But haikua hivyo coz hapokei simu zangu mpaka nikaamua nimtext ya kwamba ni mimi lakini hakunijibu nikapita insta na kumtag kwenye one of the posts zilizoandikwa mtag mtu uliye mmiss nikadhani ataresspond but kimya. Now nimeamua kumuuliza, mbona unakuwa kama mtu kwenye kinyongo na mimi ama mtu kwenye vita baridi na mimi? kama hutaki kuwasiliana nami niambie ili nikudelete kichwani mwangu though upendo wangu kwako ntashindwa kuudelete coz it goes deep nnajua ujumbe huu utakufikia (usiwe kama watu wanaotembelea nyota za wenzao na wamepewa masharti na mganga ya kuwa ukiwasiliana na unayetumia nyota yake basi umaarufu na fedha ulizonazo vyote vitapotea) samhani lakini.”

Shaa katika picha hapo chini

shaa-sugua-gaga

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez