Witnes Ashumtumu Mrisho Mpoto kumsaliti kwenye kampeni ya Uzalendo.

Witnes Ashumtumu Mrisho Mpoto kumsaliti kwenye kampeni ya Uzalendo.

Ni jana ambapo wasanii baadhi wa muziki wa kizazi kipya walishiriki katika kampeni ya Uzalendo wa utunzaji wa mazingira Mkoani Dodoma.

Mapema leo kupitia mtandao wa WhatsApp kwenye group la wasanii Witness Kibonge Mwepesi ambaye ni msanii wa hiphop ameandika “Ninajisikia nimekabwa koo kwa simanzi na masikitiko makubwa sana yenye machungu makali mpaka siwezi kuongea.

Kwa namna moyo wangu unavyoniuma nahisi machozi yakinibubujika kwa namna nilivyogeuka jiwe la kukanyagia ili watu wapite na safari zao, Je huu ni uzalendo?

Maybe uzalendo wa matabaka huo ninakubali upo. Ila mwenyezI mungu pekee ndIYo ajuae shughuli nilizo acha ili kwenda kurekodi wimbo ambao mwisho wa siku wameenda kurekodi watu wengine kabisa wamebadilisha vitu baadhi including artists.

Kasoro Mrisho Mpoto na Cassim Mganga ndo wamebaki Tumehangaika wote mpaka kwenda kwenye interview nimeacha usingizi na joto langu la pembeni. Nikasitisha hadi kushuti kipindi cha Tv kinacholeta ugali mezani mwangu ili tu kuonesha uzalendo wangu coz nina amini katika msemo *ask not what a country can do for you, ask what you can do for your country*

Ila mwisho wa siku ninapata jeraha kubwa sana la moyo ambalo sina uhakika wa kupona leo kama ni shati jeupe limeingia doa, na full kunichoresha TBC 1 live na kwenye Press conference na mbele ya Waziri Dr Mwakyembe mbele za wasanii wa tasnia zote hadi ma mc na kunitambulisha ya kwamba ni kati ya watu walioshiriki kwenye wimbo wa uzalendo wa kitaifa na nitakuwepo dodoma katika uzinduzi wa hii kampeni ya uzalendo na utaifa nchi yangu kwanza but imekwenda ndivyo sivyo.

Tena bila taarifa kama uliyeyafanya haya ni wewe Mjomba Mrisho Mpoto sawa haina shida mungu yupo ila kama yupo wa kumtupia lawama aliyeko serikalini wizarani ama kwingineko kokote kule pia sawa, ila muambie witness ameumia sana”

 

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa