WITNES AELEZA SABABU YA KUFANYA KAZI NA MPENZI WAKE

Witz_n

Sharifa ni wimbo wake Witnes Kibonge Mwepesi unaofanya vyema mara tangu kutoka kwake, Witnes ambaye ni moja kati ya wale waliokuwa wanaunda kundi la Wakilisha akiwe na wenzake kama Shaa na marehemu Langa.

Haikuwa kazi ngumu kwa Witnes kujibu swali lililoulizwa na msikilizaji katika kipindi kipya cha Ladha 3600 ndani ya efm kinachoongozwa na Jabir Saleh. Ambapo katika sagment ya Swali sindano masikilizaji alipata wasaa wa kumuuliza Witnes kuhusu kufanya kazi nyingi na mpenzi wake. Ambapo Witnes amesema “Kuna sababu nyingi ila wacha niseme kadhaa, unajua kuna wakati mtu unahitaji kuachia kazi kwa haraka na wasanii wengine wanakuwa bize hivyo ufanyaji kazi na Ochu huwa ni rahisi zaidi, pia Ochu ni mtu mwenye kipaji nadhani mnaona hata katika wimbo wa Sharifa ameonyesha uwezo mkubwa. Binafsi naamini kama ana uwezo mkubwa wa kufanya vitu viwili. Hivyo hainipi tabu kufanya nae kazi nyingi mana ni mtu mwenye kipaji cha hali ya juu.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez