Wimbo wa Mwana Fa watimiza miaka 15 tangu kuanza kuchezwa Radioni.

Wimbo wa Mwana Fa watimiza miaka 15 tangu kuanza kuchezwa Radioni.

Dume suruali ni wimbo wake unaofanya vyema ndani ya nchi na nje pia. Mwana Fa ni moja kati ya marapa bora walioko chini ya kivuli cha hiphop, ambaye tangu aingie katika ramani ya muziki wa kizazi kipya hajawahi kupoteza ubora wake.

Mwana Fa amekuwa msanii tofauti zaidi na wengine katika upande wa kutunza rekodi za muziki wake. Ni wazi changamoto moja wapo ya wasanii wa kizazi kipya ni kutokujua kutunza rekodi ya mambo yote katika muziki wao.

Kupitia mtandao wa picha ‘Instagram’ Mwana Fa ameweka wazi rekodi zake katika maisha yake ya muziki, ambapo ameeleza “2/2/2017 Ni miaka 15 ‘cash’ toka mara ya kwanza wimbo wangu umepigwa redioni..Ingekuwa Vipi feat Jay Mo produced by Bon Luv nashukuru! Lakini pia hakuacha kuweka wazi wake ambao anaupenda zaidi ambao ni ‘Mfalme’ akiwa amemshirikisha G Nako.

 

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa

Attachment