Weusi wapata dili la kuwa mabalozi wa DSTV.

Weusi wapata dili la kuwa mabalozi wa DSTV.

Weusi ni kundi la muziki ambapo kwa sasa linafanya vyema katika uwanja wa muziki wa kizazi kipya.

Ambapo mapema leo kupitia  mtandao wa picha “Instagram” Dstv wameandika “Multchoice Tanzania inayofuraha kuwatambulisha rasmi Weusi kuwa mabalozi wa DSTV, Tuendelee kulisongesha”.

Hakika ni jambo jema na zuri katika muziki huu wa hiphop na wasanii wake, lakini ikumbukwe sio muziki pekee wa Weusi ndiyo umeweza kuwapa dili bali nidhamu na kuheshimu Sanaa yao lakini watu wengi waliowazunguka.

Na msingi mkubwa wa msanii ni yale mahojiano ufanyayo ni wazi watu husikiliza kwa umakini, hivyo kama ni mtu wa kuongea hovyo yasiyo na maana huwezi kupata nafasi ya ubalozi.

Muziki,  nidhamu, dili kwa hakika tupo mahala pazuri kama makampuni yataendelea kutazama nafasi ya uhalisi wa nidhamu ya kazi.

#TuzungumzeMuziki.