“Watangazaji mnammaindi Diamond Platnumz kwa lipi?” Ncha Kali

“Watangazaji mnammaindi Diamond Platnumz kwa lipi?” Ncha Kali

Ncha Kali ni miongoni mwa watu wachache ambao wamekuwa wawazi katika kuupa ukweli nafasi yake. Na mara zote amekuwa akitoa mitazamo yenye tija na inayopaswa kuzingatiwa katika kuendeleza muziki wa kizazi kipya.

Ncha Kali alikuwa ni Mtangazaji wa Clouds Media Group miaka kadhaa nyuma katika Kipindi cha XXL na So So Fresh. Lakini sasa ameachana na kazi hiyo ya utangazaji na amekuwa akijishughulisha na shughuli nyingine.

Utofauti wake na wenzake katika kusupport vipaji vya kweli umeweza kumpa heshima mpaka leo hii, ilihali afanyi tena kazi hiyo ya Utangazaji.

Mapema leo kupitia mtandao wa Twitter hakusita kuweka wazi mtazamo wake juu Diamond Platnumz na watangazaji juu ya kauli ya Diamond aliyosema “Siwazi Radio na Tv kama sehemu ya promosheni ya muziki wangu”

Kauli imeonekana kuwagusa watu wengi wa Media,ambapo wapo waliosema hadharani ila wapo ambao hawajasema ila kuandika vijembe katika mitandao ya kijamii.

Ncha Kali kupitia mtandao wa Twitter ameandika “Watangazaji wammemind Mondi kwa lipi haswa? Wanaelewa huu mchezo unavyobadilika? Wapunguze jazba halafu watafakari kidogo”

“Watu wanapata nyimbo na videos kabla hata ya radio kuzipata! Ngoma zinabang kwenye Bhajaji kabla ya radio pendwa kuzitambulisha”

“Ni haki kwa mtu kupanic pale unahisi “kudharaulika” ila hasira hizo zizifanye ukajichoresha zaidi! #ImJustSaying”

“Ndio radio zinachangia kukuza BRAND ya msanii ila wakati umefika kwa vituo kusoma ishara za nyakati! Watu wana njia mbadala”

“Vituo vinalazimika kujiongeza ili kuonyesha umuhimu wao sio tu kwa wasanii bali pia kwa CHAPA zingine za kibiashara”

“Vijana wana point za msingi ila naona kama wamepanic kiasi na hawataki kukubali ukweli….KUNA MIANYA MINGI MINGINE”

“Radio/ tv zitabaki kuwa nguzo kubwa kwenye mpango wa mawasiliano wa CHAPA yoyote ila kizazi hiki kina mahitaji mapya ….KASI!”

“Wakati wangu redioni kauli ya Mond ningeichukulia kama tusi maana wakati ule nilikua na kasumba ya “Bila Sisi Wewe Si Kitu!”

“Ila kwa hapa nilipo na kwa yale niliojifunza baada ya kuacha utangazaji…. ILE NI KAULI ILIO NA UKWELI NDANI YAKE”

“Hili wazo kwamba mtu akiamua kufuata njia zingine za kujitangaza ni dharau…ni wazo la kishamba Sana”

“Narudia Tena. …nyakati zimebadilika.. communication channels zimeongezeka….na zote zinatakiwa kujiongeza kuendana na dunia mpya”

Je shabiki una mtazamo gani? kabla ya www.tizneez.com kutoa mtazamo wetu muda wowote kutoka sasa.

Tupe maoni yako hapa

Facebook Tizneez

Twitter Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez