Wasanii watuhumiwa dawa za kulevya wafikishwa mahakamani

Wasanii watuhumiwa dawa za kulevya wafikishwa mahakamani

Wasanii watuhumiwa 10 wa dawa za kulevya ambao ni wale waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wameshafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu asubuhi ya leo.

 

Katika kundi la  wasanii kutoka katika muziki na bongo muvi ni Rommy Jones, TID, Babuu wa Kitaa, Petit Man, Tunda (model wa kike), Lulu Diva, Recho, Joan, na wengine.

Watuhumiwa wamesomewa kiapo cha Mahakama ambapo pande wa Jamuhuri umeomba watuhumiwa hao waamrishwe kuwekwa chini ya uangalizi kwa kuripoti polisi mara 2 kwa mwezi kwa kipindi cha miaka 2 ili kuangaliwa kama wameacha tabia ya kutumia dawa hizo hususani bangi
Lakini wakili wa upande wa utetezi anamedai taarifa hizo hazijakamilika kwani hazioneshi wanaojiusisha na dawa za kulevya na walikamatwa lini na wapi na hakuna ushahidi wa kujitosheleza wa madai hayo kiasi cha wao kupata dhamana ya kuangaliwa tabia zao bila polisi kutoa ufafanuzi wa kina wa kwanini wanahitaji kupata dhamana ya uangalizi wa nidhamu.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa

Attachment