Wasanii wajifunze kwa Chege, Temba na Said Fella

Capture

Wasanii wajifunze kwa Chege, Temba na Said Fella

Team tizneez ilitamfuta meneja Maneno ambaye ni moja kati ya mameneja ambao ameweza kuwa na wasanii wengi. Sam wa ukweli, Rich Mavoko na Nay wa mitego ni moja kati ya wasanii ambao aliwahi kufanya nao kazi.

Napenda watu wajifunze kuhusu Fella na Chege na Temba wapo zaidi ya miaka 10. Unajua kuibuka kwa makundi mengine pale Tmk ingekuwa ni wasanii wengine hakika wangeshagombana. Ila wale jamaa wanafahamu kazi.

Ila katika sababu ambazo zinafanya wasanii kuachana na sisi mameneja au kuachana meneja yoyote yule ni msanii kujiona mkubwa, pia vitu kadhaa vinambadilisha. Pia msanii kuona kuwa ana mashabiki wengi na hakuna tena mtu wa kumzuia kufanya kitu hivyo hilo hupelekea kuachana na meneja wake huku akisahau kule ambapo umemtoa.

Kikubwa ni msanii kuheshimu mtu ambaye amekutoa mbali ni vyema kuwa na uvumilivu. Siachi kusema wasanii wajifunze kwa Chege na Temba pamoja na Saidi Fella.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez