Wasanii waandika ujumbe kwa Sugu, baada ya hukumu.

Wasanii waandika ujumbe kwa Sugu, baada ya hukumu.

Sugu ni Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye ni zao halali la muziki wa hiphop lakini ni msanii aliyepigania muziki huu kiasi sasa kuwa sehemu ya ajira kwa vijana wengi.

Mapema leo Mahakamini Jijini Mbeya amepewa hukumu katika kesi yake iliyokuwa ikimkabili juu ya kumtolea Rais Magufuli maneno ya fedheha.

Hukumu yake ni  kutumikia kifungo cha miezi 5,na wasanii mbalimbali wameandika  jumbe mbalimbali katika mitandao ya kijamii baada ya hukuma hiyo.

Msanii Rama Dee yeye kupitia mtandao wa picha Instagram ameandika “Nasikitika sana kwa hii habari kama Msanii pia kama Rafiki Wa Sugu,hii si picha nzuri! ”

Izzo Bizness “Stay strong Big Brother JONGWE “

Lakini Nikki wa Pili ameandika “Nguvu ya Mungu ikapate kuwa nawe pamoja na familia yako, gerezani sio kaburini stay strong Jongwe “

Mwisho.

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa