WASANII WAAMUA KUFANYA TAMASHA LA WAZI(DEMOCRACY IN DAR)

Wakati tukielekea uchaguzi mkuu October mwaka huu 2015 kumeendelea kuwa na matamasha mabalimbali ambayo yamekua yakitoa elimu juu ya kuchagua viongozi bora na sio chama.Kitu ambacho kimeleta zaidi utofauti ni wasanii wengi kutoka katika tasnia mbalimbali wamekua wakijitoa katika kueleimisha watu juu ya uchaguzi na umuhimu wa kupiga kura.

 “Democracy in Dar” Tamasha kubwa na la wazi litafanyika siku ya jumapili tarehe 16-8-2015 katika viwanja vya Mbagala Zakhem kuanzia saa 7 mchama hadi 12 jioni. Njoo ushuhudie katika stage ya uhakika na mziki mnene vitakavyotumika kudondosha bonge moja ya burudani toka kwa: Florah Mbasha Kala Jeremiah Profesa Jay Ney wa Mitego Juma Nature Roma Mkatoliki Msaga Sumu Mkoloni na Sugu bila kusahau upande wa bongo movie watakuwepo Haji Adam aka Baba Haji  Jacqline Wolper Auntie Ezekiel – Shamsa Ford  Jimmy Mafufu: Mbali na hao wapo pia wachoraji katuni maarufu na wawakilishi wa sanaa nyinginezo. Tamasha ni bureeeeee. Ni jumuiko la wasanii na sio umoja wasanii tumejumuika na kutoa burudani tu   ,Alisema msemaji ambae hakutaka jina lake liwewazi kwasasa.

kuwa karibu na sisi kwa kutufuata katika mitandao ya kijamii

facebook.com/tizniz

instagram tizneez

twitter team tizneez.