“Wasanii wa kike wasio na vipaji vya kuimba wamejua kucheza na akili za watangazaji”

“Wasanii wa kike wasio na vipaji vya kuimba wamejua kucheza na akili za watangazaji”

Jambo la kutaka kuwa na jina kubwa kwa maana ya umaarufu linakua zaidi upande wa watoto wa kike. Ambapo sasa idadi yao katika muziki wa kizazi kipya imezidi kuongezeka siku baada ya siku, kila mmoja anataka kuimba vile ajuavyo yeye.

Ila katika uhalisia wenye vipaji vya kweli ni wachache mno, wengi wao ni wazugaji na hutumia zaidi miili yao katika kubaki nusu uchi ilihali tu waweze kuzungumziwa katika media na mitandao ya kijamii.

Maana watangazaji katika upande wa burudani wengi wao si watu wa kusifu ubunifu katika muziki ila kusifu muonekano wa msanii zaidi tena akiwa katika mavazi ya nusu uchi.

Kama watangazaji wangekuwa ni watu wa kusifu ubunifu wa kazi basi hakika tungeona nyota ya Grace Matata ikiwa juu zaidi, lakini kwa vile anajiheshimu na kutengeneza muziki mzuri basi ni amekuwa ni kikwazo kwa watangazaji walio wengi, maana  wasiojua vipaji na muziki mzuri ndio wamekuwa wakiamini kuwa ndio wajuaji (Watangazaji)

Katika kukua kwa sumu ya mambo ya ajabu zaidi tumeona hata msanii Dayna Nyange nae kuingia katika kundi la wasanii wakike ambao sasa wameamua kutumia miili yao ilihali tu waweze kuzungumziwa zaidi.

Picha ya Dayna Nyange chini hapa itazame

Capture

Dayna Nyange katika picha juu

Ncha kali ya jambo hili linachoma muziki wa wasanii wengine wazuri wenye vipaji vya kweli, maana wasio na vipaji wamejua namna ya kucheza na akili za watangazaji wengi.

Ila siachi kuwaambia wasanii wenye vipaji wakisitashwe tamaa na wasanii wachache wasio na vipaji ambao wametawala sasa katika media nyingi, maana “Mnywa maji kwa mkono mmoja kiu yake ipale pale”

Ifike mahala

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube Tizneez