Wasanii ni vyema mkafuata nyayo za Best Naso

Wasanii ni vyema mkafuata nyayo za Best Naso

Team Tizneez imeweza kufika katika kisiwa cha Ukara ambapo ni moja kati ya visiwa 37 ambavyo vipo kwenye ziwa Victoria, ikiwemo na kisiwa cha Ukerewe ambacho ndicho kisiwa maarufu Zaidi ilihali pia ni Wilaya ambayo ipo ndani ya Mwanza.

Moja ya mambo ambayo tumeweza kuyajua ni kwamba licha ya Ukara kuwa ni moja kati ya visiwa vidogo lakini ni moja ya sehemu ambayo muziki wa kizazi kipya umeweza kufika vyema.

Na msanii pekee ambaye ameweza kwenda na kuchukua hela zake katika kisiwa hiki na vingine vya karibu ni Best Naso. Kwa hakika katika sehemu nyingi tuendazo hasa za vijijini hukuta jina la Best Naso likiwa limetawala midomoni mwa watu na kuambiwa yakuwa “Mara nyingi huja hapa na tunampenda sana, akija lazima watu wajae kumuona akifanya tumbuizo”

Kiuhalisia kuna cha kujifunza kutoka kwa Best Naso kwa maana ya wakati wasanii wakilalama juu ya kukosa matamasha mengi ya mjini yaliyojaa ushikaji na kuimbishwa bure mwenzao Best Naso amekuwa akiifuata pesa yake kwenye vijiji vingi ambavyo matamasha mengi makubwa hayafiki.

Ni wazi muamko wa muziki wa kizazi kipya ni  mkubwa mno katika maeneo mengi mno, hivyo wasanii ni vyema kufuata nyayo za Best Naso katika kuendeleza maisha yao Zaidi.

#TuzungumzeMuziki.