Walter Chilambo Ajibu kauli ya Nay wa Mitego kwa vitendo

IMG_2327

Walter Chilambo Ajibu kauli ya Nay wa Mitego kwa vitendo

Ni mshindi wa Bss miaka kadhaa nyuma. Ambaye ni wazi uwezo wake wa kufanya muziki uko katika kiwango cha juu.

Maneno yalikuwa mengi hata msanii wa Ney wa mitego aliposema “Namuona Walter Chilambo kapigika kama zamani” haya alisema katika wimbo wake wa salaam zao.

Mapema jana Walter amezindua studio yake yenye viwango vya kimataifa zaidi, ambapo ni wazi kuna sehemu za kurekodi mambo tofauti tofauti. Studio hiyo ina ukubwa kiasi cha kuchukua hata wasanii zaidi ya 50 kwa mara moja katika chumba cha kurekodia sauti. Lakini pia studio hiyo ina sehemu maalum kwaajili ya kurekodi matangazo tu.

Ni wazi studio hii ndiyo studio kubwa sasa hapa Tanzania.

Team tizneez inakupongeza Walter kwa kufikiria mbali zaidi.

SOMA HAPA JINSI TEKNOLOJIA INAVYOPIGA TAFU MZIKI WETU

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez