Wakazi aandika andiko juu ya kikao cha wasanii cha kisanii kilichofanyika juzi.

Wakazi aandika andiko juu ya kikao cha wasanii cha kisanii kilichofanyika juzi.

Kupitia mtandao wa picha Instagram msanii wa hiphop Wakazi hakuacha kuweka wazi maoni yake juu ya kikao lakini kujibu dhihaka za Steve Nyerere juu ya wasanii ambao hawakuweza kufika.

Wakazi ameandika  “TOILET PAPER (StINAPO LICHEKA DODOKI!!

Moja ya vitu ambavyo vimeirudisha sanaa ya nchi yetu nyuma ni ufanywaji wa shughuli kiholela, kimihemuko, kwa maslahi binafsi, bila kujali PROFESSIONALISM.

Inasikitisha STEVE NYERERE (Mpaka leo sijui ni msanii wa kitu gani, ila najua ni Mwana Siasa wa CCM kwa uhakika) kuwabeza watu ambao wamejaribu kusisitiza mambo kufanywa kiutaratibu unawaita Madodoki.

Well, sir you are FULL OF SHIT, kama Toilet paper. Ilitakiwa uyavae mapungufu yako kama mratibu na kusema next time utafanya marekebisho sio kuwatukana. Mimi mwenyewe sikupata taarifa na ni moja ya wasanii ambao tupo very active kwa sasa.

Mwaka Jana wakati Sekretariet ya Chama Cha Mapinduzi ilivyotaka kuongea na Wasanii, simu zilipigwa na mialiko ilitolewa na Humphrey Polepole. Sasa sisi ndio tushobokee kikao chako kisa Mkuu wa Mkoa, unaumwa nini?!

Kwanza wewe na Mkuu wa Mkoa mna mandate gani ya kuongelea Sanaa wakati Waziri husika yupo (Mwakyembe) BASATA ipo, Shirikisho la Muziki lipo, na Vyama husika vipo. Msituletee mambo yenu ya holela holela hapa na agenda zenu binafsi kupitia Sanaa. Kwanza hamna jipya lolote mliloongea.

Kama mnataka kupeana michongo peaneni huko huko, muwaache wasanii tuendelee kutaabika na shida zetu. Uratibu wa Misiba sio sawa na Wa wasanii. Au nikuulize huyo Mkuu wa Mkoa anataka wasaidia wasanii wa Dar tu na Waliopo Instagram au?!

Mbona TCRA walitoa wito kwa wasanii kwenda kwenye kikao, wiki nzima na walitumia viongozi wa vyama?! Kuweni Professionals, na fanyeni mambo kiutaratibu kama kweli ni kwa maslahi ya wote, ila kama ni michongo yenu fanyeni kimya kimya kama ilivyo kawaida. Na mkiniudhi nitamuandikia Barua Rais Magufuli kuwasemea..!!”

Ameandika Wakazi.