Wakati Vannesa Mdee akihitajika kituoni, Wema Sepetu, Tid, Nyandu Tozi na Babuu wa kitaa waendelea kushikiliwa na Polisi

Wakati Vannesa Mdee akihitajika kituoni, Wema Sepetu, Tid, Nyandu Tozi na Babuu wa kitaa waendelea kushikiliwa na Polisi.

Ni jana ndio ilikuwa siku ya kuitikia wito wa Mkuu wa Mkoa Mh Paul Makonda, kwa wasanii na watu wengine maarufu, Ambao Mh aliwataka kufika kituo kikuu siku ya jana bila kukosa juu ya mambo yote yanahusisha tuhuma za madawa ya kulevya.

Wema Sepetu, Tid, Nyandu Tozi, na Babuu ni baadhi ya wachache ambao  waliitikia wito wa Mh Paul Makonda.

Na katika wasanii wote ambao walifika kuitikia wito huo wa Mh Makonda wameendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi. Kamanda wa polisi Kanda maalum Dar Es Salaam Simon Sirro amethibitisha hilo.

Lakini pia msanii Vannesa Mdee ametakiwa kufika bila kukosa siku ya jumatatu ya tarehe 6/2/2017, pamoja na video queen Tunda.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa

 

Mwisho

Attachment