WAANDAAJI WA VIDEO TANZANIA KAZENI BUTI

SONY DSC

Mziki wetu umekuwa na mabadiliko makubwa sana tofauti na miaka ya nyuma, kipindi hicho msanii moja kati ya ndoto  zake kubwa ilikua ni kurekodi katika studio kubwa kama Mj record, Bongo record, Sound crafters, na Kama kawa record mbali na hapo ni kufanya collabo na wasanii waliokua na majina kwa kipindi hicho.

Swala la video halikua na asilimia kubwa sana katika muziki wao, kwani hata waandaaji wa video  kipindi hicho hawakua na umaarufu wala ukubwa wa majina. Isipokuwa maprodyuza wa nyimbo tofauti na ilivyo kwa sasa .hapo tusiitumie sababu ya teknolojia sababu nchi kama kenya na Uganda walikua wanafanya video na zikawa zinapata airtime katika vituo vya hapa kwetu.

Walio yaona mapungufu ya mziki wetu katika suala la video hawakutaka kuona tunabaki palepale kwani game lilikua gumu la video mpaka makampuni ya utengenezaji wa video ya G2 production na Royal production yakapotea kabisa katika ramani.
Na kufikia hatua ya wasanii wa hapa nyumbani kusogea nchi jirani kwenda kufanya video, miaka ya 2009 wasanii walibadilika sana katika muziki wao na kuvutiwa na suala la utengenezaji wa video na Kipindi hicho waandaaji walikua na ubunifu uliowashawishi wasanii wengi na Pamoja na kuvutiwa na waandaaji wengine wadogo kuichukulia fani ya uandaaji wa video ni ajira kama zilivyo ajira zingine katika mziki huu wa  Kizazi kipya hapa nawazungumzia Adam juma wa Next level na John Kallage
Walioingia kwa nguvu katika utengenezaji wa video.

Kadri siku zilivokua zinazidi kwenda na ndio thamani ya video inaongezeka  na waandaaji wa video wameongezeka na kufanikiwa kujulikana nje ya mipaka yetu na kazi zao kuchezwa katika vituo vikubwa hapa afrika hii itawafanya waandaaji wadogo kukaza buti na ili wazidi kuongeza idadi ya waandaaji bora kabisa kwa afrika.

Kwani naamini Tanzania tuna vipaji vingi katika upande huu wa video.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

NA JOHN SIMWANZA