VYAMA VYA SIASA VILIPASWA KUWAPA ELIMU WASANII KABLA YA KUWATUMIA.

98758769219241386275tanzanya
MWAKA huu 2015 ni mwaka tofauti kabisa katika uchaguzi mkuu tangu kunzishwa kwa vyama vingi.Mfumo wa vyama vingi ulianzishwa mwaka 1992 ambapo ulitoka katika mfumo wa chama kimoja ambacho kilikuwa Tanu ambacho kilianzishwa mwaka 1954 na baadae mwaka 1977 ikaja kuwa (CCM)Chama Cha Mapinduzi.
Mfumo wa vyama vingi ulianza rasmi kutumika mwaka 1995 ambao ndio ulikuwa uchaguzi wa kwanza kushirikisha vyama zaidi ya kimoja katika uchaguzi.Na uchaguzi mwingine ulifuta mwaka 2000,2005,2010 na sasa 2015.
Ambapo mpaka sasa chaguzi zote za vyama vingi imeweza kutoa marais watatu ambao n Rais msataafu Ally Hassan Mwinyi,Benjamin William Mkapa na Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ndiye anayemaliza muda wake mwaka huu.Lakini mpaka sasa Tanzania imeshaongozwa na maraisi wanne ambapo Rais wa awamu ya kwanza alikuwa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Uchaguzi wa mwaka 2015 ambao mpaka sasa bado haujatangaza rasmi rais wa awamu ya tano lakini kuna baadhi ya majimbo tayari yameshatangazwa majina ya wabunge ambao wamepewa ridhaa na wananchi kwenda kuwawakilisha katika Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Licha ya kuwepo vyama vingi katika uchaguzi huu wa 2015 lakini hiki kipindi cha kampeni tunaona mchuano mkali kati ya chama tawala Chama Cha Mapinduzi na Chadema chini ya mwamvuli wa (UKAWA) ikiwa na maana ya Umoja wa katiba ya wananchi.Mgombea urais wa CCM ni Dk john Pombe Magufuli na wakati Chadema akiwa ni Edward Lowassa Ngoyai.Na mpaka sasa Tume inaendelea kutangaza matokeo wanayopata kutoka sehemu tofauti tofauti lakini bado haijtangaza rasmi mshindi ni nani.
Licha ya watu wengi kuzungumza kuwa uchaguzi huu utaendelea kubaki wa kihistoria hasa katika mvutano wa viongozi katika ngazi zote kuanzia udiwani,ubunge na urais.Lakini pia utabaki kuwa wa kihistoria katika tasnia ya sanaa.Mwaka huu ndio mwaka pekee ulishirikisha wasanii wengi katika kuzunguka na wagombea wa nafasi za urais katika maeneo tofauti tofauti wakati w a kampeni.
Mfumo wa kutumika wasanii au watu maarufu katika uchaguzi sio jambo geni hata katika nchi zilizoendelea,tumewahi kuona hata Marekani msanii JAY Z na Young Jezzy walijitokeza na kumfanyia kampeni Rais wa Marekani Obama,.na wapo wasanii waliokuwa wanamfanyia kampeni mpinzani wake na Obama.
Mwanzoni mwa kampeni tumeona vituko vingi tu,ikiwa n baadhi ya wasanii kuhama kutoka chama hiki na kwenda chama kingine.Licha ya kuhama tu, tumeona pia wasanii wakiacha kumfanyia kampeni mgombea wake na kuanza kutoa kashfa kwa mgombea mwingine?je unadhani ilikuwa ni kazi yao?au hawakuwa wanajua majukumu yao?nadhani jukumu lao ilikuwa ni kushawishi jamii yake kumchagua mgombea wake na sio kutoa kasfa au maneno yasiyofaa juu ya mgombea mwingine.
Wakati tume ikien delea kutoa matokeo ya urais kuna baadhi ya wasanii wanaendelea kupost matokeo katika mitandao ya kijamii.Na wengine wamekuwa wakipost picha zenye kuendele kutoa kashfa kwa mgombea mwingine.Je hili hawaoni kama linaweza kuhatarisha amani,maana ni upotoshaji wa hali ya juu.Nilitarajia kuoana wakati huu hao wasanii/watu maarufu wakiandika vitu au kupost vitu vyenye kutuunganisha watanzania na sio kuendelea kuandika mambo ambayo yanaonekana wazi yanaleta uchochezi wa uvunjifu wa amana.Kwasababu tayari kampeni zilishaisha na hata akishinda nani atakuwa rais wa watanzania wote.
Maana hata hao wabunge walioshindwa katika majimbo mabalimbali wamekuwa wakitoa kauli zenye kuonyesha umoja wa watanzania.Sasa wewe msanii/wasanii/watu maarufu msiojua maana ya siasa ndio mnashangaza watu.Siasa sio vita siasa sio chuki.
Nafikiria vyama husika vilipaswa kuwapa elimu juu ya siasa, Iko wazi wengi wanachanganya maisha yao binafsi na siasa.Sasa yawapasa kujua ni rahisi sana kuvunja amani kupitia wao kulingana na kile wanachokiandika katika kurasa zao za mitandao ya kijamii.
Wasanii msichange maisha yenu binafsi na siasa,Siasa ni njia ya kufanya maamuzi katika mji,taifa na hata dunia.Ni vyema kuandika vitu vinavyowaunganisha watanzania sio kuwagawa.
Mungu ibariki Tanzania
Instagram/TIZNEEZ
Twitter/TIZNEEZ
Facebook/TIZNIZ