VITALI MAEMBE NA MAWAZO TOFAUTI JUU YA SIKU YA UHURU NA USAFI

10983419_1599366313608284_3004310748487957575_n
Vitali Maembe ni muimbaji wa nyimbo za asili mwenye maskani yake Bagamoyo mkoani Pwani.Sumu ya teja ni moja kati ntimbo kubwa zilizompa umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi pia.Licha ya kufanya mziki lakini Vitali amekuwa akifanya matumbuizo ya mtaani akiimba nyimbo za kueleimisha jamii akitumia gitaa lake kufikisha ujumbe.
Kupitia ukurasa wake wa faceboo Vitali Maembe ameandika”Mh. Rais! Wazo zuri lakini siku sio yenyewe Baba!
Tangu Tanganyika ipate Uhuru ni miaka 54 sasa lakini tangu izikwe bila kufa ni miaka 50 sasa!
Nikiwa naitafakari Furaha ya waliokuwapo siku ya Jumamosi ya Tarehe 09/12/1961
Kuishusha Bendera ya Mkoloni na Kupandisha Bendera ya Tanganyika Huru!
Najipa moyo nakamata Beleshhi langu, nakamata Fagio na Reki najaribu kuvitumia vyote kwa pamoja, lakini naishiwa nguvu!
Bhabha!
Inawezekana ikawa ni kweli sina sababu ya kusherehekea Uhuru wa Nchi yangu lakini haiwezekani nikawa sina sababu ya kutafakari Uhuru wangu!
Mzanzibari ana haki ya kujiita Mzanzibari na kukataa kujiita Mtanzania Visiwani, lakini mimi nalazimishwa kujiita Mtanzania Bara na nikijiita Mtanganyika naambiwa ni dhambi, dhambi ya kukataa Muungano.
Bado tu sina haki ya kutafakari Uhuru wangu?
Niitumie siku hii tukufu kushika taka na kuziweka upenuni na kuzitazama nikitafakari wapi pa kuzitupa kwakuwa kuna Amri ya kusafisha lakini hakuna pa kutupa taka? Hakuna majalala rasmi kila unapotaka kutupa unaambiwa usitupe hapo na ni kweli hapafai kutupa, Tumezibua mitaro na maji taka bado hayaendi mifumo ya maji taka na maji safi yote imefumuka, mimi leo siutafakari Uhuru wangu na wala sina uwezo Wa kutafakari kingine zaidi ya taka.
Nafikiri Mimi wacha nijifanye kuwa nimeielewa hivi hii Fasihi ya Mheshimiwa Rais, kwamba…
‘Tusafishe Moyo yetu, Tuzibue mitaro na mabomba/mifereji ya fahamu na Akili zetu, ili tuwe Huru kweli kweli’
Watanganyika!
Ikumbukwe kuwa, Kwa sababu za kisiasa, na siri sirini Muunganoni tunalazimishwa kuiita Nchi yetu “Tanzania bara” na sisi kujiita Watanzania Bara badala ya Watanganyika ingawa wengine tupo Mafia na Kilwa kisiwani.
Hatukumwaga Damu lakini Tumetumia Damu! Hatukutumia Mtutu Wa Bunduki lakini tumetumia Akili na Jasho.
Tanganyika ilikuwa eneo linalotawaliwa na Uingereza kuanzia 1919.
Baadae Wazee wetu walipambanaTanganyika ikawa nchi huru,
Uhuru ambao haukupatikana Kwa kumwaga damu lakini kwa Kuitumia Damu na Jasho.
Uhuru uliodumu kati ya 1961 hadi 1964.
Uhuru na Unchi uliodumu Kwa muda mfupi kuliko.
Wazee wetu walipitia vipindi vigumu!
Baada ya Biashara za Utumwa, kudhalilishwa na kunyanyaswa kwa miaka na mikaka! Walikuja Wajerumani na Manyanyaso yao, kisha Mwaka 1919 sehemu kubwa ya koloni la Kijerumani ilikabidhiwa rasmi mikononi mwa Uingereza kama eneo la kudhaminiwa chini ya mamlaka dhalimu ya Shirikisho la kishenzi la Mataifa kulingana na kifungu 22 cha mkataba dhalimu Wa Kizungu.

Mwaka 1922 Shirikisho la kishenzi la Mataifa lilithibitisha hatua hiyo na kuamua masharti ya kukabidhi.

Waingereza walihitaji jina jipya kwa ajili ya koloni hilo na tangu Januari 1920 wakaamua kuliita Bustani ya Tanganyika “Tanganyika Territory” kwa kutumia jina la ziwa kubwa upande wa mashariki mwa Afrika.

Nimechanganyikiwa!
Bado nashindwa kuamini kuwa nahitaji Kuutafakari Uhuru wangu Kwa kuzoa taka? Na sio kujiuliza kwanini wenzetu wana Bendera, Serikali, Wimbo Wa Taifa, Bunge, Katiba na Mamlaka na sisi tunanyimwa!
Tena Bado katika siku 366 za mwaka mmeiacha Valentine Day, X day, E day na I day nimechaguliwa ‘Uhuru Day’ iwe siku yangu ya kutafakari Taka?!!? Ni
Twitter@tizneez
instagram @tizneez
facebook@tizniz