Vitali Maembe Atoa ujumbe kwa Naibu na Baraza lake

12494953_1711970652347849_1221865737804632706_n

Sumu ya teja ni wimbo wake uliompa umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi.Hata hivyo Vitali Maembe ni moja kati ya wasanii ambao tungo zao hugusa jamii moja kwa moja.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook hakusita kuweka wazi hisia zake ambapo ameandika “Mh. Waziri, Naibu na Baraza! Hamuwezi kuonekana warefu kwa kuwakata vichwa warefu zaidi yenu, Kuvaa miti muwe kama Ngongoti ingesaidia kidogo, lakini hamna kipaji hicho. Labda ningewashauri mpande juu ya Sturi muonekane warefu!

Msisafirie nyota za wasanii, Andaeni mazingira na mfanye kazi yenu kwa Maadili ya kazi husika Taifa liwe na Heshima na Adabu! Msiwavizie, Mnaacha watu wakosee, mlopoke hadharani muonekane mnafanya kazi!
Aibu yenu!

Mimi ‘Mswahili Flani’

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez