VIPANDE 4 CHONGANISHI VYA VIDEO YA NEY WA MITEGO

Vipande Gomvi Vya Nay
Ni siku kadhaa zimepita tangu kutoka kwa video ya shika adabu yako ya msanii Ney wa mitego, ambapo wimbo huo ulifungiwa baada ya wiki kadhaa tu tangu kutoka kwake na BASATA. Licha ya wiki kadhaa msanii Ney wa alionekana akiandika katika mitandao ya kijamiia akiandika kuhusu kufanyika kwa video hii, na hata kupata wasaa mzuri wa kwenda katika media moja kati ya nyingi akiendelea kutambukisha wimbo huo ambao tayari ulishafungiwa. Team tizneez ilimtafuta msemaji wa BASATA lakini hakukuwa na mafanikio ya kumpata, maana ni kitu kinachoshangaza nyimbo kufungiwa na baadhi ya media zimeendelea kuucheza.
Video ya shika adabu yako imetoka na sasa imeenea katika kila Blog ndani na hata nje ya nchi. Katika video hiyo kuna vipande kadhaa ambayo ni wazi ni vipande tata na chonganishi ambayo kwenye jamii sidhani kama vitaleta maana nzuri, ingizikatiwa Rais wa SHIMUTA Shirikisho la Muziki Tanzania alisema “Nitasimamia nidhamu katika sanaa nitahakikisha wasanii wanafanya sanaa ambayo inajenga jamii” Je kwa hili la Ney linajenga jamii?
Kipande kimoja wapo kati ya vile vinne ni kipande kinachomuonesha mtu aliyejifanya/ kujivisha uhusika kwamba ni Shetta akipewa funguo ya gari na bosi ambaye kuna mtu alivaa uhusika wa Chief Kiumbe ambapo baada ya kupewa funguo ilionekana akishikwa makalio,na mtu aliyevaa uhusika wa Shetta alionekana kufurahi kwa kitendo hicho, je hii inaleta maana gani katika jamii?
Kipande kingine ni kipande kilichomuonesha mtu mwingine aliyevaa uhusika wa Ray kigosi ambaye wiki kadhaa alionekana kushika akili za walio wengi katika mitandao ya kijamii juu wa weupe wake. Katika video hii ameonekana mtu aliyevaa uhusika wa msanii Ray kuonekana akiwa anakunywa maji na mtu mwingine ambaye alivaa uhusika wa mama kuonekana kama kushangazwa kama sio kumfokea kwa kile anachokifanya.Je kipande hiki kina manufaa?
Kipande cha tatu ni cha Ommy Dimpoz ambapo katika kwa mara ya kwanza tu wimbo ulipotoka nae hakusita kuonesha hisisia zake kwa kile alichoambiwa na Ney “huyu jamaa anaitwa dimpoz poz kwa poz wanae wanalalamika hawamjua shemeji kitaani kuna tetesi mwana hapigi mechi mara ooh jogoo hawiki wonyeshe shemeji” kwa jambo kama hili wewe unaona ni sawa? Nadhani wasanii hawajui kama wao wanayo nguvu ya kuaminika zaidi katika mitaa, yaweza kuwa alifanya kupata vina ila je wengi wao wanajua kama alifanya kwa kutaka vina? Licha ya Dimpoz kuonekana kujibu katika mtandao wa picha Instagram, lakini sidhani kama nguvu ya jibu lake katika kujitete itaenda kama ilivyokwenda wimbo wake msanii Nay. Katika video ameonekana mtu aliyevaa uhusika wa Dimpoz akiingia chumbani na msichana na watu kuchungulia dirishani. Lakini jamaa waliochungilia walionekana kushangazwa kuona kuwa jamaa hakufanya kitu, sijui maana halisi ya sehemu hii ilikuwa nini?
Kipande cha mwisho ni kipande cha mwana dada Wema Sepetu ambae ameonekana mtu aliyevaa uhusika wake ambapo alionekana kama ni mtu aliyeweka vitu kama nguo kwenye tumbo lake ili aonekane mwenye ujauzito.
Nini maoni yako katika haya? Tupe maoni yako hapa
www.tizneez.com
Twitter tizneez
Facebook tizneez
Instagram tizneez
Youtube tizneez