VANESSA MDEE ATOA NAFASI ZA KAZI

AFRIMA-2015-Nominee-Vanessa-Mdee

Moja kati ya wadada ambao wanafanya vizuri katika ramani ya bongo fleva huwezi kuacha kumtaja Vanessa Mdee a.k.a Vee Money. Closer ni wimbo wake uliomtambulisha vyema na hata kumpa tuzo ya KTMA 2013-2014.

Kupitia mtandao wa picha Instagram Vanessa Mdee alipost na kuandika “Dancers Je wewe ni Dancer mzuri na uko tayari kucheza na mimi katika matamasha mbali mbali? Karibu kwenye audition za wazi zitakazo fanyika Jumapili hii pale NAFASI ART SPACE MIKOCHENI. #ComeDanceWithVee kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi na mbili jioni”

Swala la kuwa Dancer imekuwa kazi kama ilivyo kazi nyingine, ambapo sasa imeonekana  kuwa ni kiungo muhimu kati ya msanii hasa katika show zake za kila siku.