Vanessa Mdee Ajibu tuhuma za Edu Boy

Vanessa Mdee Ajibu tuhuma za Edu Boy

Edu Boy ni moja kati ya wasanii wachanga walioibuka mwaka 2015 -2016 ambapo ukaribu wake na Young Killer ulifanya kufahamika zaidi. Maana alikuwa akipata nafasi ya kushiriki jukwaani na Young Killer katika matumbuizo mengi.

Licha ya baadae Edu Boy na Young Killer kuingia katika majibizano ambayo kila mmoja alieleza akivuta upande wake.Ambapo mpaka kuisha kwa tatizo lao hakuna chembe ya ukweli iliyojulika a.

Mapema leo Eddu Boy alipokuwa anatambulisha wimbo wake wa Nairee aliomshirilisha Bill Nas Alisema “Sio lazima mtu ku’post cover ya ngoma yangu lakini nilimpigia simu Vanessa Mdee akanimabia nisimsumbue na cover zangu”

Kupitia mtandao wa Twitter Vanessa Mdee amejibu kwa kuandika “Sawa Edu Boy pokea kicki yako jombaa. Ya Juu Kabisa tena hii ni zaidi ya cover” Vanessa akaongeza kwa kuadika “Wiki hii naona nimekuwa wakusingiziwa tu. Edu Boy huyo huyo niliyomfanyia backing vocals kwenye wimbo wake wa kwanza”

www.tizneez.com

Instagram Tizneez

Twitter Tizneez

Youtube Tizneez

Facebook Tizneez

 

Source Xxl Clouds Fm