Uongozi wa Chama cha muziki wa kizazi kipya waeleza madhara ya madawa ya kulevya.

Uongozi wa Chama cha muziki wa kizazi kipya waeleza madhara ya madawa ya kulevya.

ATHARI/MADHARA YA MADAWA YA KULEVYA KATIKA JAMII.

Dawa za kulevya ni nini?

Takwimu za sensa ya taifa ya watu na makazi ya mwaka 2012 zinaonyesha kwamba idadi ya vijana nchini Tanzania ni 15,587,621 sawa na asilimia 34.7 ya watanzania wote. Idadi ya wasanii kwa sasa inakadiriwa kuwa ni zaidi ya milioni7 sawa na nusu ya vijana wote nchini.

Dawa za kulevya ni kemikali ambazo zikitumiwa hubadili hisia, fikra na tabia ya mtumiaji.

Pia dawa za kulevya ina maana ni matumizi mabaya ya dawa na hasa pale yatumikapo kinyume cha maelekezo ya tabibu na hivyo kuleta madhara kwa mtumiaji.

Tatizo la dawa za kulevya nchini limeendelea kukua licha ya jitihada mbalimbali

zinazofanyika katika kupambana nalo. Hali hii inadhihirishwa na kiasi kikubwa cha dawa za kulevya kilichokamatwa nchini hususan heroin na cocaine katika siku za hivi karibuni

Aina za dawa za kulevya

Tunatofautisha dawa za kulevya katika makundi mawili. Zile zinazokubalika na zile zisizokubalika kisheria.

Tanzania, dawa za kulevya zinazokubalika kisheria ni pamoja na tumbaku na pombe, pia dawa zilizothibitishwa kwa maandishi na daktari. Dawa zinazotolewa kwa udhibitisho wa madaktari ni zile dawa za kutibu.

Pale zinapotolewa kwa sababu nyingine mbali na matibabu au maelezo ya daktari zinakuwa dawa za kulevya. Miongoni mwa dawa zinazotumika vibaya hapa Tanzania ni valium, asprin na panado. Vimiminika kama petroli pia hutumiwa kama dawa za kulevya. Vitu hivi hutumiwa kwa njia ya kuvuta hewa yake kwa pua au mdomo.
Pia kuna vileo visivyoruhusiwa ambavyo hutengenezwa kienyeji kama vile gongo.

Dawa za kulevya ambazo hutumika sana Tanzania ni pamoja na bangi, mirungi, mandrax, heroini na kokaini.
Njia nyingine ya kuzungumzia dawa za kulevya ni kutokana na madhara yake. Yapo madawa ambayo hupagawisha au yanayozubaisha au kupoozesha kama vile kileo, nikotini, dawa za usingizi, kwa mfano valium na heroini. Dawa hizo zinamfanya mtumiaji kujisikia shwari au fresh, lakini pia huhuzunisha. Dawa zinazochamngamsha ni  kama mirungi, kokaini na zile za kuvuta, kwa mfano petroli, zina madhara ya kukufanya uhamasike na kujisikia kuwa na nguvu. Dawa zinazopagawisha zinaleta hisia, sauti, taswira, harufu kwa mtu japokuwa vyote hivyo havipo kweli. Mfano mmoja wapo ni Bangi.

Dawa za kulevya inachochewa na mambo mbalimbali yakiwemo

mmomonyoko wa maadili katika jamii, tatizo sugu la rushwa, uchu wa kutaka utajiri wa

haraka, uelewa mdogo wa athari za dawa za kulevya na ukosefu wa ajira. Aidha, kuwepo

kwa mfumo dhaifu wa udhibiti husababisha kushamiri kwa biashara na matumizi haramu

ya dawa za kulevya nchini. Matumizi hayo huathiri afya za watumiaji, kudhoofisha

nguvukazi ya Taifa na kuongeza umasikini. Vile vile, biashara hiyo huchochea uhalifu wa

aina mbalimbali ukiwemo wizi, ujambazi, ubakaji na rushwa.

 

Matumizi ya dawa za kulevya kwa sasa ni mojawapo ya changamoto kubwa

zinazoikabili dunia. Changamoto hii ipo katika nchi zote maskini na tajiri, ikihusisha

makundi na rika zote katika jamii duniani na Tanzania tukiwemo.

 

Kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2011, inaonyesha Mikoa ilio athirika zaidi na matumizi ya dawa hizi ni mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Arusha, Mwanza, Mbeya, Iringa na Morogoro ambapo wengi wa watumiaji ni vijana wa wenye umri kati ya miaka 12 na kuendelea.

(sio wasanii tu)

Madhara ya matumizi ya dawa za kulevya ni makubwa na yanajidhihirisha katika

nyanja zote, kiafya, kiuchumi, kijamii, kisiasa, kiusalama na kimazingira pia.

 

Aidha, watumiaji wa dawa za kulevya wanakadiriwa kuwa kati ya 150,000-500,000 na zaidi kwa hapa nchini huku waathirika wa ukimwi wanakadiriwa kuwa zaidi ya milioni mbili. Ipo hja pia kupiga vita ukimwi kwa nguvu zaidi ya dawa za kulevya.

 

Mtumiaji madawa ya kulevya anaweza kubainika kama ametumia dawa ndani ya siku 30 tangu ache kutumia kwa mara ya mwisho.

 

SHERIA

Katika miaka ya 90, Serikali ilianzisha vitengo vya kudhibiti dawa za kulevya katika baadhi ya idara na taasisi zake ili kuimarisha jitihada za udhibiti wa dawa za kulevya. Taasisi hizo ni Jeshi la Polisi, Idara ya Usalama wa Taifa na idara ya Ushuru wa Forodha.

Pamoja na jitihada hizo, tatizo la dawa za kulevya limeendelea kukua ambapo mwaka 1995, Bunge lilitunga Sheria ya Kuzuia Biashara Haramu ya Dawa za Kulevya Namba 9 ya Mwaka 1995 [Sura 95].

Sheria hiyo ilianzisha Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya ambayo ilianza kazi mwaka 1997, chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Kwa mujibu wa Sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya (the drug control and enforcement act, 2014) ilipitishwa na bunge Machi 24, 2015.

Sheria hiyo inasema kuwa watakaobainika kufanya biashara haramu ya madawa ya kulevya watozwe faini ya sh. Bilioni moja au kifungo kisichopungua miaka 30.Aidha atakayekutwa analima, kusambaza mbegu, kusafirisha, kuzalisha au kuingiza mimea inayozalisha dawa za kulevya kama bangi, mirungi na cocaine atatozwa faini isiyopungua sh. Milioni 20, kifungo kisichozidi miaka 30 au vyote kwa pamoja

WITO

Tunashauri serikali kuhakikisha harakati za kudhibiti upatikanajiwa na matumizi ya dawa za kulevya ziendane sambamba na harakati za kuwapatia dawa za matibabu waathirika wa madawa hayo na huduma mbadala. Ukizingatia kuwa vituo vya matibabu ni vichache sana na baadhi ya maeneo yaliyo athirika hayana huduma hizo kabsa.

Pia nawakumbusha kuwa jukumu la kupambana na dawa za kulevya ni letu sote. Hivyo

tuunganishe nguvu zetu ili kukabiliana na tatizo la biashara na matumizi haramu ya dawa

za kulevya. Ni wajibu wetu tukiwa vijana, raia wazalendo kufanikisha azma ya kujenga Taifa

lisilo na biashara wala matumizi ya dawa za kulevya.

 

Tunaomba serikali iweke mkazo zaidi katika janga hili, itoe elimu, udhibiti, tiba kwa miongoni mwa vijana walio athirika na isiishie kwa kuwatangaza tu na kuchafua majina yao, tunafahamu wasanii wengi wetu wanaaminika na kufanya vizuri sana Africa na Duniani kwa ujumla.

 

Kwa kuwaongelea vibaya wasanii hao ni kituhuma ni kuiongelea vibaya nchi yetu kwa ujumla. Tasnia hizi ndio zenye uwakilishi mzuri wa Taifa duniani kwa ujumla na ukichafua majina yao ni sawa na kuichafua nchi pia. Kukamatwa kwao watuhumiwa si lazima kuwatangaza ila tungependa watangazwe wahukumiwa na si wa tuhumiwa ili iwe fundisho kwa watumiaji na wauzaji wa madawa hayo ya kulevya nchini.

 

Imeandaliwa na Katibu wa Tuma Ndugu Samuel Mbwana (Braton)